Utapataje Pesa Nguvu zako zikiisha?

… …Kwa mujibu wa utafiti uliowahi Kufanya na mtaalamu Michael Bukwimba kuhusu wastaafu wa Tanzania…

…ilionekana kuwa 86.49% ambao wanategemea pensheni peke yake wako kwenye hatari ya kufa haraka mara baada ya kustaafu.

Maisha yana majira ambayo unatakiwa kuyatumia kimkakati.

Kuna majira ambayo utakuwa na NGUVU na MUDA wa kutosha kuzalisha.

Ila kuna majira yatafika, hautakuwa na nguvu kabisa za kuzalisha.

Kama leo unatumia NGUVU na MUDA wako kupata pesa…

…Ina maana lazima uanze kuweka mikakati pale siku ambapo nguvu zako zitakuishia utakuwa unaingiza pesa kwa NJIA GANI.

Imeonekana kuwa 81% ya wastaafu ambao walikufa miaka 8 baada ya kustaafu (2007-2015) ni wale ambao…

…pension yao kwa mwezi ilikuwa kati ya 50,000/= hadi 100,000/=; na ilikuwa haitoshelezi mahitaji yao.

Ili kuepuka mtego huu, Jitahidi uanze mapema kutenga pesa…

…kwa ajili ya uwekezaji ambao utakuja kukusaidia siku ambapo nguvu zako zimeisha.

Tafuta maeneo ambayo unaweza kuwekeza na ukapata rejesho (Income Producing Assets)…

…ili utakapofika huo UMRI ambao wengi wanateseka, wewe UWE SALAMA.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment