Mungu alimchagua Musa aende kuwaokoa wana wa Israel kutoka utumwani lakini Musa alikua na visingizio vingi; akamwambia Mungu mimi sijui kuongea,(Musa alikua na kigugumizi) pia alikua muoga akijua alitoka Misri kwa kukimbia alikua akitafutwa kwa makosa aliyo yafanya,alijiona hana nguvu za kupambana na Farao.Mungu yeye aliangalia ndani ya Musa yaani roho yake aliona kuna ujasiri,aliona kuna hekima,aliona kuna nguvu.Hata wewe leo hii Mungu ameweka mpango ndani yako kupitia wewe utakomboa familia yako,utakomboa ndoa yako,utakomboa jamaa na rafiki zako acha kujiwekea vizingizio na kujiona huwezi hakika nakwambia hapatakuwepo mtu kama wewe duniani tena wa kuifanya kazi ambayo Mungu kaiweka kwako,Mungu hutumia vinyonge kuviangusha vyenye nguvu sio kwamba alishindwa kumponya Musa akaweza kuongea vizuri hapana alitaka akajitukuze kwa Farao aone Mungu ni wa ajabu sana akamwambia nenda utakutana na Haruni atakuwa anaongea badala yako.Hata wewe yuko mtu anao mtaji wako anakusubiri yuko mtu anataka kubariki maisha yako acha kuhuzunika na kujiona huwezi simama na uanze tena utakutana na Mungu na atakuinua.
Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.