Unachokitafuta kuna mtu anacho tayari na…
…pia wapo wengi wanaokitafuta kama wewe.
Moja ya kitu kinatofautisha tabia zetu ni kiwango cha “Njaa”…
…ulichonacho kwenye kila unachokitafuta.
Watu wenye njaa, huwa hawafanyi mambo kwa sababu ni marahisi…
…au wana muda, HAPANA.
Huwa wanafanya kwa sababu HAWANA MBADALA.
Yaani, ukiona wewe unaacha kwa sababu kuna upinzani…
…unasusia kwa sababu haujapata Matokeo uliyotarajia,
Yaani, ukijikuta unapata shida kuamka mapema ili ukimbizane na ndoto zako…
…au ni Kama vile unalazimishwa kufanya hiyo kazi/biashara/Kusoma; basi Ujue BADO HAUJA NJAA.
Sikiliza, Kama hauna Njaa Ya kiwango cha JUU kwenye unachofanya…
…uwe na uhakika hautapata MATOKEO YA JUU.
Kufanya kitu bila kuwa na NJAA ya kutosha ni KUPOTEZA MUDA.
Tafuta kitu ambacho kinakukosesha UTULIVU Kisha uweke 100%…
…Hapo badala ya kufanya ambacho hauna HAMASA NACHO.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.