Likomboe Taifa lako!!!

Ni Wakati Wa Watu Wakuu Kuinuka Kwenye Taifa…

Kwenye kila Taifa huwa kuna MAJIRA ya kuinuliwa watu MUHIMU kwenye kizazi cha wakati huo…Danieli alifanyika bora Havana aliyehudumu katika serikali tofauti maana alifahamu kusudi la Mungu katika kizazi chake,Yusufu aliota ndoto,na kutafsiri tuu kunampa hadhi Kuu,Daudi aliona mwanya na huo ukawa mwanzo wa ufanisi wake,Modekai anamkumbusha Esther usipowasaidia Hawa wateule was Mungu,Mungu atamwinua mtu mwingine,kutoka mateso wanayopitia mikononi mwa Hamani,kuna kitu Mungu anakiandaa,usiwe mfano wa Gidioni anayekwepa majukumu Hadi malaika anamkumbusha wewe shujaa.Usiogope. Hebu tazama Deborah Mwanamke wa kawaida tuu anainuliwa kuwa jaji na nabii katika Taifa la Israel.

…WATAKAOACHA ALAMA miaka ya MBELE wanajiandaa leo..Panda mbegu Leo mavuno yatakuja. Usiile mbegu yako ukiona wengine wana sherekea mavuno yao.

Yaani, ukisoma HISTORIA za mataifa mengi utagundua kuna “pattern”…

…ya namna watu WAKUU wanavyoinuliwa kwenye kila kizazi (Generation).

Ukisoma historia ya Kenya, Tanzania,Uganda na barani Afrika na duniani kwa ujumla tazama uwiano wa Idadi ya watu tangu uhuru (Population Structure)…

…hakuna UBISHI kuwa, sasa ndio Kipindi ambacho hao watu WANAINULIWA.

Uzuri ni kuwa, ukifika kwenye MAJIRA haya NAFASI zinakuwa SAWA.

Majina MAPYA YANAINUKA Kwenye Sanaa, Biashara, Siasa, Vyombo vya Habari n.k

Gundua eneo lako, jikite hapo kwa NGUVU ZOTE.

Kumbuka, NGUVU yako ya kesho kwenye TAIFA itatokana na uwekezaji unaofanya leo,jiandae leo kwa ajili ya kesho…

…kwa WATU Kwenye ENEO lako ULILOITIWA.

Wewe unajiandaa kuwa MKUU kwenye eneo lipi katika TAIFA LAKO?


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment