Unapojitoa zaidi ya wengine!!!

Ni kweli kuna wengine HAWAJITOI kama wewe UNAVYOJITOA.

Kuna wakati unaweza kufika hatua ukaona kama vile UNAJIUMIZA sana…

…ukilinganisha na wengine.

Yaani unatumia NGUVU na MUDA mwingi kupambania mambo yako…

Kufanya kazi ofisini… …wakati wengine ni kama WAMESHARIDHIKA.

Usisahau, NDOTO ZENU HAZIFANANI.

Ili upate kile ambacho wengine HAWAJAKIPATA…

…ni lazima uamue KUFANYA vile ambavyo wengine HAWAJAVIFANYA.

Yaani, ukusudie kuwa utaenda “Extra-Mile” ili uwe “Extra-Ordinary”.

Ukifanana na wanavyoishi leo…

…basi utafanana na MATOKEO wanayoyapata kesho.

Ni zile hatua za ZIADA ambazo huwa UNAZICHUKUA ambazo wengine WANAOJIHURUMIA…

…Huwa hawazichukui ndio zitakufanya uwe TOFAUTI.

Jikague, ni kitu gani ambacho unafanya kilicho TOFAUTI na wenzako…

…ambacho kitakuongezea THAMANI LEO?

Kama Umejifunza Kitu Comment Neno “Mimi ni wa Kipekee”.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment