Jitahidi Uwe Sehemu Ya Mkuu Anapokuwa Kwenye MCHAKATO.
Watu wengi sana huwa wanasubiria mtu afike JUU kwenye…
Biashara, Kipaji, Uongozi n.k…
…ili waanze kutengeneza mahusiano imara, ni kosa la kimkakati.
Mentor wangu mmoja aliwahi kuniambia “When You Help Someone Bigger Than You, It Makes You Part of Something Bigger”
Akimaanisha: Unapomsaidia mtu ambaye ana hatima kubwa kwenye eneo Fulani…
…tayari na wewe unakuwa sehemu ya kitu kikubwa kitakachokuwa mbeleni”.
Usisahau hili, kwenye kila MAJIRA ya maisha yako…
…MUNGU atakukutanisha na watu waliobeba UKUU kwenye eneo fulani.
Jitahidi KUWEKEZA kwao kwa kufanya vitu VITAKAVYOWAINUA.
Wasaidie Kifedha Kama unaweza…
…Wasapoti katika wanachofanya ambacho kwao ni cha Thamani.
Hivi ndivyo unavyonunua HISA kwenye UKUU wao wa kesho.
Usipofanya hivyo, utaishia kusema.
“Yaani, namfahamu sana. Tulikuwa wote, Ila sasa hivi AMENISAHAU”.
Wekeza Kwenye Maisha Ya Watu Kimkakati KABLA HAUJACHELEWA.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU”
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.