Mwanzo 13:12 Abram AKABAKI nchini Kanaani na Lutu akakaa kati ya miji iliyokuwa bondeni, AKAHAMISHIA KAMBI yake Sodoma.
Baada ya LUTU kuona amefanikiwa na ameanza KULINGANA na ABRAM kiutajiri na JINA kuwa kubwa, aliamua kuhamisha kambi.
Kuna kitu ALISAHAU, kwa namna Mungu alikuwa ameyaweka maisha Yake, BARAKA na USALAMA wake ulikuwa unategemea MAHUSIANO Yake ya KARIBU na ABRAM.
Alipoamua kujiondokea, baadaye YAKIMKUTA MAAFA na ABRAM ndiye alikwenda KUMSAIDIA tena ili KUMUOKOA.
Uwe makini, kuna watu MUNGU anakuunganisha nao hata baada ya kuwa UMESHAFANIKIWA hutakiwi KUTENGANA nao kwa sababu WAMEBEBA kitu kwa ajili yako.
Usimpoteze ABRAM wako kwa kuona MMESHALINGANA, wengine unawahitaji zaidi baada ya kufanikiwa kuliko kabla haujafanikiwa.
Nakutakia Jumapili Njema.🙏🙏🙏
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.