Wafahamu watu hawa watano!!!

https://youtu.be/69iBkNmDzus?si=MmFPjY2YTKSpGSrm
Je, Wewe Unao Hawa WATU WATANO?

Hivi ni nani ATABAKIA na WEWE?

Wako wengi ambao wanafurahishwa na KICHEKO chako.

Kuna wengi ambao wanavutiwa na FURAHA yako.

Swali ambalo ni muhimu kujiuliza:

“Hivi ni nani ambaye ANAYATHAMINI machozi yako?”

Unapokuwa na MAUMIVU makali na kupitia MAGUMU…

…Unapokuwa umebakia peke yako, Nani anayahisi MAUMIVU yako?

Pale ambapo umepoteza kila ulichonacho kilichowafanya watu WAKUPENDE:

Cheo, Mali, Nafasi, Umaarufu, hivi ni Nani atakabakia na wewe?

Umeshawahi kuwaza kwa bahati mbaya umepata AIBU ambayo…

…ikashusha HESHIMA yako na kuharibu JINA LAKO, Jamii haitaki kukuona tena:

Hivi katika MAJIRA hayo, Nani ATAENDELEA kusimama na wewe?

Wapo wengi wanaambatana na wewe kwa sababu UNASHINDA kwenye unachofanya.

Vipi siku UKISHINDWA na UKAPOTEZA, Nani ataendelea kuwa na WEWE?

Leo, TAFAKARI: Hivi unaweza kuandika majina ya watu 5 ambao una uhakika…

..Kama kila mtu ATAKUKIMBIA, wao wataendelea KUSIMAMA na wewe?

Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU”


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment