Hekima uwezo wa kukitumia unachokijua kwa usahihi!!!


Mwanzo 41:33 “Basi, Farao na AJITAFUTIE mtu wa AKILI na HEKIMA amweke JUU ya NCHI ya Misri”.
.
Nafasi yoyote ya UONGOZI kwenye level ya nchi kwenye SEKTA yoyote ile (Biashara, Siasa, ofisini, Sanaa, afya n.k); lazima mtu awe na vitu hivi VIWILI.

AKILI: Ni uwezo wa KUCHAMBUA mambo mbalimbali kwa HARAKA na kujua UHUSIANO wake ili kujua mbinu za kutumia ili kupata FAIDA au kuzuia HASARA.

HEKIMA: Uwezo wa kutumia ulichokijua kwa USAHIHI ili kikuletee matokeo CHANYA.

Ukimpata mwenye akili ila hana hekima, atavutia kwa MANENO yake ila hatakuwa na MATOKEO. Ukimpata mwenye hekima “kidogo” (Hasa inayotokana na uzoefu), atakuwa na MBINU nyingi nzuri ila hatakuwa na uwezo wa kuleta matokeo ya kudumu yanayoendana na NYAKATI.

Unaona YUSUFU alivyomwambia mfalme? “JITAFUTIE”. Yaani kwanza SIO KAZI RAHISI kupata mtu mwenye vyote viwili. Pili, hii kazi ni lazima mwenyewe AHUSIKE, sio ya kuchaguliwa kwa niaba.

Mtu yeyote anayesimamia chochote kwa LEVEL ya NCHI, ni muhimu atimize VIGEZO hivi viwili.

Ukijaza wenye akili peke yake KILA SIKU utakuwa unatatua MATATIZO yanayotokana na TABIA na MAAMUZI yao. Ukijaza wenye hekima peke yake kila siku itakuwa ni VIKAO visivyoisha kujadiliana maamuzi sahihi ni yapi.

Ukikosa mwenye vyote viwili, tafuta wawili ambao kila mmoja ana kimoja kwa kiwango cha juu.

Nakutakia Jumapili Njema


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment