Watu wengi ambao UMRI wao UMEENDA sana, nilipokutana nao wamekuwa na MAJUTO YANAYOFANANA.
Yaani, wengi wao HAWAJUTII sana kwa MAKOSA waliyofanya, kwa sababu walipata muda wa KUYAREKEBISHA au ilikuwa ndio “best decision” waliyoweza kulingana na UFAHAMU wao wa wakati huo.
Wengi wanajutia MAMBO AMBAYO HAWAKUYAFANYA.
Yaani, wanatamani vile vitu ambavyo WALIVIGHAIRISHA kuvifanya kwa sababu ya HOFU au kuogopa watu WATASEMAJE, wangekuwa na UJASIRI wa kuvifanya.
Wanagundua kuwa, kulikuwa na watu wengi kama wao, wenye VIKWAZO na MAZINGIRA yanayofanana, ila wenzao walikuwa WAJASIRI.
Hata wewe, leo kuna FURSA unazo, kuna maamuzi unajua unatakiwa kuyafanya, ila bado UNAGHAIRISHA.
Unachotakiwa kujua ni kuwa, kuna UMRI ukifika HAUTAWEZA TENA KUFANYA.
Fanya leo kinachopaswa kufanywa leo, ili kesho USIJIKUTE UNAJUTIA UZEENI.
Muda wowote ukiwa tayari nikusaidie kutimiza malengo yako hizi ndio namna 4 ninazoweza kukusaidia.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.