Jiulize swali Kila siku!

Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple, Steve Jobs aliwahi kusema kuwa…

…kila siku asubuhi alikuwa anajiuliza swali…

“Kama leo ingekuwa siku yangu ya mwisho kuishi, ningeishi kama ninavyopanga kuishi?”

Kila unapoamka asubuhi lazima uwe na na kitu UNADHAMIRIA kukikamilisha.

Usiamke bila MALENGO maalumu unayotaka kuyakamilisha kwenye maisha yako.

Leo umepewa dakika 1,440 na sekunde 86,400, utazitumiaje?

Siku zote kumbuka hili “Wake up with Determination and Go to bed with Satisfaction“.

Amka ukiwa na Dhumuni fulani la kutimiza ili ukienda kulala leo uwe umeridhika.

Kuna jambo gani ambalo leo unapanga kulifanya…

…ili utakapokwenda kulala uwe umeridhika moyoni mwako?

Usikubali leo uipoteze kama ulivyopoteza siku zingine.

Ishi kwa namna ya tofauti.

Na hili ndilo bao la asubui.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment