Pepo mchafu amtokapo mtu hukimbilia mahali pasipo na maji akitafuta mahali pa kupumzika.
Neno hili lina maana fulani ambayo itakuwa msaada kwako kama ukielewa vyema
Unaposikia habari kama hizi haimaanishi mapepo huishi jangwani hapana Maji ni “NENO”.Kabla hujapata neno la Mungu unafananishwa na mtu mwenye kiu,Yesu akasema yeyote atakaye kunywa maji yangu hataona kiu milele,Neno la Mungu ni uzima mtu anapo pokea Neno hilo kwa imani na kulishika mapepo hukimbia na kumuacha huru.Kumbuka hata tukiomba huwa hatunywi dawa bali kupitia neno tu wagonjwa wanapona,kupitia neno tu maisha yako yanabadilika,kupitia neno unapokea baraka ndipo uanze kujua anayefunga na kuharibu maisha yako ni pepo mchafu lakini ukimuamini Mungu na kila jambo lako litakua sawa nami natamka kila linalokuzuia kwenye maisha yako likakutane na Moto wa Roho mtakatifu neno hili likamkimbize pepo wa aina yeyote aliye zuia maisha yako
Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.