Wengine hawakumis niuchokozi tuu!!

Sio kila ANAYEKUCHOKOZA ili UONGEE ni kwa sababu AMEKUMIS.

https://youtu.be/69iBkNmDzus?si=MmFPjY2YTKSpGSrm
Kuna wengi ambao WANATAFUTA neno kutoka kwenye kinywa chako, ili waje walitumie kinyume NAWE.

Ni Calvin Coolidge aliywahi kusema “Silence Can Never Be Misquoted”, yaani hakuna anayeweza kuongeza/kupunguza maneno kwenye sentensi ambayo HAUJAISEMA.

Kuna wakati USHINDI wako hauko kwenye KUONGEA, bali uko kwenye UKIMYA WAKO.

Kuna watu wanatafuta USEME kitu ambacho baadaye watakitumia kama USHAHIDI. Kuna wengine wanataka “Kuprove” kitu fulani, wanatamani UONGEE ili wakamilishe DHAMIRA YAO.

Haujawahi kuona kuna watu wanaulizwa kitu bila kujua kumbe wanarekodiwa na baadaye inawagharimu?

Vivyo hivyo, UKICHOKOZWA usiwe mwepesi KUONGEA kwa HASIRA. Ni MTEGO HUO. Waache watafsiri UKIMYA wako kuwa ni UOGA, ila kwako ni HEKIMA.

Nakuombea, Mungu akupe HEKIMA ya KUTOKUONGEA pale unapopaswa KUKAA KIMYA.

Muda wowote ukiwa tayari nikusaidie kutimiza malengo yako hizi ndio namna 4 ninazoweza kukusaidia.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment