Ukiwa karibu na mtu mwenye “Low Self-Esteem”, unaweza kujikuta kwenye shida kubwa sana.
Yaani aidha awe MWENZI wako, BOSI wako au MBIA wako kwenye BIASHARA, bado ni tatizo.
Moja ya kitu kibaya sana ambacho watu ambao wana “Low Self-Esteem” hukifanya ni kumtreat mwingine vibaya (Mistreatment).
Yaani ile hali ya wao kukosa kuiona THAMANI YAO wenyewe, huwa wanaitafuta kwa KUMKANDAMIZA mwingine.
Hawa ndio wale ambao, utashangaa kila siku anatafuta namna ya KUKUNYANYASA, kukusemea maneno MABAYA ili AKUUMIZE n.k
Kiufupi ni kuwa, huwa anatafuta KUIPATA thamani yake kwa KUONYESHA wengine kuwa HAWANA THAMANI.
Ukiwa na mtu wa namna hii, uwe makini sana, kwa sababu USIPOKUWA mwangalifu na wewe UTAPOTEZA HALI YAKO ya KUJIAMINI na KUJITHAMINI.
Ukigundua ANASUMBULIWA na “Low Self-Esteem”, usibebe maneno na matendo yake moyoni.
Usianze kutafuta MAKOSA yako na UDHAIFU wako, HAUTAONA, yeye ndiye MWENYE MATATIZO. Enjoy Life.
Umejifunza kitu?
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA KITU”
TheHeartBeatofAfrica
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.