Ndivyo Sivyo!!!

Huu Nao Ni Moja Ya Ukweli Mchungu Niliowahi Kuambiwa Na Mtu Mwenye Hekima.

Baada ya kuweka nguvu kubwa sana nikiamini nitapata nilichotaka…
.
…Baada ya kusubiria kwa muda mrefu.

Baada ya kuona kila dalili inaonyesha kuwa nilichokuwa nakisubiria kimeshakuja GHAFLA KILA KITU KINAENDA NDIVYO SIVYO.

Mtu huyu mwenye hekima akaja akaniambia “Sometimes You Don’t Get What You Want Because You Deserve Better”
.
(Wakati Mwingine Haupati Unachokitaka Kwa Sababu Unastahili Kitu Bora Zaidi Kuliko Hicho Unachokitaka).
.
Mimi hii imenikuta mara nyingi sana.

Kuna wakati unataka kitu au kuonana na mtu fulani kwa nguvu sana ukiamini itakuwa ni baraka kubwa sana kwako.

Ghafla, inashindikana.

Unaanza KULAUMU, unaanza KULAANI.

Baadaye unakuja kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni lazima ukose hiyo fursa/hicho kitu ili UPATE BARAKA KUBWA ZAIDI zilizoko MBELE YAKO.

Yaani, unakaa hadi unasema “Mungu naomba unisamehe kwa kunung’unika, sikujua kama ulikuwa UNANIEPUSHA NA HATARI…
.
…Sikujua kama Ulikua UMENIANDALIA JAMBO ZURI/KITU KIZURI NAMNA HII”.
.
Hata wewe inawezekana leo uko kwenye maumivu ya kumkosa mtu au kitu.

Badala ya kulalamika, amua kushukuru.

KUNA KITU/MTU MZURI SANA YUKO MBELE YAKO.

TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment