Siku moja Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana,akamwambia Yakobo, Tafadhali,naomba chakula nile kwa kuwa ninazimia mimi.Yakobo akamwambia Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.Esau akakubali, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.Yakobo akampa Esau mkate na chakula akala, akanywa.Esau na Yakobo walikua ni ndugu wa tumbo moja mkubwa Esau na mdogo Yakobo siku moja Esau akapatwa na shida ambayo ilitaka kugharimu maisha yake akaenda kwa Yakobo ili amsaidie,Kuna wakati unaweza kuona watu wanakupita tu kimaendeleo,wanakupita tu kimaisha ukadhani Mungu amekusahau,hapana Mungu ana mahesabu yake watu wa mwilini kama Esau wenyewe utumia nguvu katika kutafuta wanaamini akili zao na sio Mungu,lakini watu wa rohoni kama Yakobo wao wanamuamini Mungu na wanakua na nia thabiti ndani ya mioyo yao ipo siku yule aliyekuwa anakudharau na kuona unapoteza muda kwenda kanisani,unapoteza muda kumuomba Mungu atakuja anashida kubwa,atakufata akiwa mgonjwa akihitaji Mungu wako amponye,atakufuata akiwa ana matatizo ya familia yake akitaka Mungu wako amsaidie ndipo utakapo anza kuringa na Mungu wako utajisifu na kumwambia Mungu wangu anaweza na utampa mkate wa uzima na maji ambayo ni Neno la Mungu kwaajiri ya kumsaidia kwenye shida yake ya Rohoni.Neno hili likakutie Nguvu jiamini na ujue Mungu atawafanya adui zako wapige magoti na kuomba msaada kwako ndipo nawe utachukua mali zako zote walizo kuibia na kuziteka.
#Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates
All rights reserved©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.