Leo tutaangalia kuhusu the power of focus. Hauwezi ukapata ukuu kama haujajikita kwenye focus. Na ndio maana watu wengi ambao ni very bright, wanaweza kuishia kuwa watu wa kawaida. Focus ni muhimu sana, una concentrate kwenye kitu kimoja. Unaweza kukuta mtu, anacho kidogo tu, ila anafocus na kukifanya kiwe kikubwa. Anajua akicheza tu ndio maisha yake yameenda mrama. Focus inaleta Perseverance – kukomaa.
Maana ya focus:
1.Focus ni kuchagua eneo moja tu, ambalo unahisi strength yako iko hapo, halafu unawekeza rasilimali zote ulizonazo.
Yaani unaachana na mambo mengine, unakomaa na hilo moja tu. Rudi nyuma sikiliza episode ya ufanye nini ili uweze kung’aa. Kwenye swala la maono, tuliongelea kuhusu kuwa na direction- na kutolea mfano wa Simba akishamchagua swala anayemuwinda.
Akishaanza kumkimbiza huwa ana focus na huyo tu. Hata akikutana na swala wengine njiani, huwa habadili Mawazo, yeye anafocus na yule tu aliyemuwinda.
Ukisoma pia kitabu cha Deep Work cha Carl Newport ameelezea sana kuhusu focus, ambapo anasema High Productivity = intensity of focus multiply by time spent. Ni muhimu ku focus kwenye kitu fulani kwa muda fulani. Siyo leo umeshika hiki, kesho umehamia kwenye kingine. Mpaka watu wanashindwa kuelewa wewe unafanya nini hasa.
2.Focus pia uinahusisha, Kutokuvutwa na kitu kingine, zaidi ya kile ulichokichagua. Yaani chochote kitakachokatiza hakitakusumbua. (rejea mfano wa simba hapo juu). Kiukweli kila field huwa inalipa. Na ndio maana kuna madaktari wamefanikiwa, na kuna ambao hawajafanikiwa. Kuna wakulima wamenikiwa na wengine hawajafanikiwa.
Sasa wewe kama ni daktari, focus kwenye kazi yako. Usije ukapewa stori za mkulima aliyefanikiwa ukatupa koti, unaenda kwenye biashara ya mazao. Utapoteza focus.
3.Focus inakutaka, kuacha kila kitu kwa ajili ya kitu kimoja. Huwezi kusema ume focus kwenye kitu fulani, kama haujaacha vitu vingine. Mfano mwanajeshi anayetaka kupanda cheo, lazima aende kambini, akafanye mafunzo, afocus ili aweze kufanikiwa. Watu hawatampata kama walivyozoea. Na wewe unatakiwa ujue, ukiaza kufocus, kuna gharama pia ya kutokupatikana kwa urahisi.
4.Focus pia, inakutaka kuaacha kuwa mtu wa hapa na pale. Huwezi kuwa ambaye kila mahali upo, halafu unasema unafocus. Na ndio maana kwenye kitabu cha Deep Work – anasema hata kama nafasi siyo yako kujibu email unaacha. Kuna watu hata email akiwekwa cc, kwamba imetumwa kwako yeye aione tu awe na taarifa, lazima atataka mpaka aijibu. Hiyo ianharibu focus.
5.Jambo lingine, ni kuachana na kila fursa inayopatikana. Kama nilivyosema hapo juu kila field huwa inalipa. Ila wewe lazima uangalie wapi ambapo maono yako yapo. Wapi ambapo strength yako ipo. Halafu focus hapo. Si kila mtu anatakiwa awe mfanyabiashara. Si kila kitu kizuri, kwa macho ni kitu sahihi kwa ajili yako. Na si kila kitu kizuri kwa mwingine, ni kitu sahihi kwako. Chukua kile ambacho ni sahihi kwako.
Unapokuwa na focus, vitu vitatu vinatokea.
(i) Inaongeza kasi
Unakumbuka kuhusu swala la maono- ukiwa na focus, unakuwa na mwanga mbeleni, unawekeza rasilimali zako zote kwenye ile sehemu ambayo unaamini strength zako zipo. Watu wanaokosa focus, wanashindwa ku focus sababu, wanatapanya rasilimali sehemu tofauti tofauti. Kasi huwa inaongezeka pale unapokuwa na focus.
(ii) Focus inajenga Brand.
Brand inakuwakilisha. Watu wanakutambuaje. Unapokuwa na focus ni rahisi sana kujenga Brand. Brand inafanya watu wakutafute. Watu wanakuelezea kwa brand yako. Brand inakupa thamani. Focus inajenga brand kwa haraka sana. Watu wanafanya biashara na wewe sababu ya vitu vitatu. Ama wanakupenda, ama wanakujua ama wanakuamini. Focus inajenga brand, brand inajenga trust.
(iii) Focus inakuondoa kwenye majuto
Inasaidia kutopoteza muda. Watu wanajutia sana kwa sababu walishindwa kufocus kwenye kitu fulani. Inasemakana watu wengi huwa wanajutia sana kwa kutokufanya mambo kuliko yale waliyoyafanya. Focus inasaidia kuwepo kwenye sehemu sahihi kwa muda mrefu, ambapo itaepusha majuto.
Maadui wa focus
(i) Wrong association (Kuambatana na watu wasio sahihi).
Siyo kila mtu anayekuja kwenye maisha yako, ataleta baraka. – watu ambao watakufanya uwe busy na maono yao, na ukaacha maono yako. Usahau maono yako, uende kwenye maono yao. Uache focus yako. Pili, watu ambao watakutambulisha kwenye vitu vizuri, na unakuta unaacha maono yako. Tatu, watu ambao wataku influence ufuate mienendo yao.
Mwisho wa siku unaingia kwenye mistari yao. Most people are born as original but die as copies. Na hii yote ni sababu ya kufuata maono ya watu wengine na kupoteza focus zao.
(ii) Indecision (Kutofanya Maamuzi)
Ukiwa mtu wa kutofanya maamuzi, huwezi kufocus. Watu wengi hawafanyi maamuzi sababu wanaogopa kupoteza, au kuogopa aibu, au kuogopa gharama. Watu wengi hawajafanya maamuzi, na wanakosa focus.
(iii) Comparison and competition with others (Kujilinganisha na Kushindana na wengine).
Hauwezi kuwa focused, kama kila siku unajilinganisha na wengine. Wewe una mbio zako, lakini unataka kujaribu kila saa kujilinganisha na kushindana na wengine. Una maono yako, hakuna haja ya kujilinganisha wengine. Winners focus on winning not on others. Usipokuwa bora zaidi ya jana, haijalishi nani yuko mbele yako, utajikuta unakuwa wa mwisho. Don’t work to be the first, work hard to be the best than yesterday. Mfano; unaweza kushindana na watu kuspend fedha, wakati hujui namna wanavyopata fedha.
#TheHeartBeatofAfrica
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.