Marufuku ya Shisha Nchini Kenya

Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Kithure Kindiki ametoa maagizo ya kuzuia uagizaji,utengenezaji,uzaaji,utumizi au matangazo ya shisha ni kinyume cha sheria nchini Kenya.Maagizo hayo yanafuatia wiki nzima ya uvamizi na kamata kamata ya Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni Dhidi ya Matumizi Mabaya ya Pombe na Madawa ya Kulevya, NACADA, kwenye vituo mbalimbali nchini Kenya.

Kenya ilitekeleza marufuku kamili ya Shisha mwaka 2017, na ikawa nchi ya nne Afrika Mashariki kupiga marufuku Shisha, baada ya Uganda, Tanzania na Rwanda.

Waziri pia alisema ni marufuku kufungua Baa wakati usiokubaliwa, na watumishi wa umma hawaruhusiwi kumiliki baa.

TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment