
Kila sehemu kuna watu wanang’aa kuliko wengine.
Hata nyota angani kuna nyingine huwa zinang’aa zaidi ya nyingine. Watu hawang’ai sababu ya kuwa wanataka kung’aa. Unang’aa sababu kuna kitu uliwahi kuvifanya. Yaani maamuzi yako ya leo ndio yatafanya ung’ae huko mbeleni. Kuna funguo unatakiwa uwe nayo ili uweze kung’aa. Na hii funguo ndio tunasema ni Maono. (vision).
Kama umewahi kuona kwenye company’s profile yoyote lazima inakuwa na mission, vision, core values na , Moto vitu vingine. Hiyo kauli mbiu ndo muhimili mkuu.Iwapo kampuni yoyote, inakuwa na maono, basi hata mtu unatakiwa uwe na maono.
Maono/vision – Ni picha ya kesho yako, ambayo imedhihirishwa ndani ya moyo wako. Wanadamu hatuna tu haya macho ya nje, ila kuna yale maono ya ndani, yaani kuna vitu huwa unaviona hata kama umefunga macho.
Macho ya ndani yanaona kuliko hata macho haya ya nje.
Maono ni sheria, bila maono ni ngumu sana kuweza kufika kule unapotaka. Bila maono unakuwa hauna direction, fursa, zinakuwepo lakini hauwezi kuzigrab, sababu tu hauna maono. Kuna misconceptions ambazo huwa watu wanaamini kuwa ndio zinawafanya wasisonge mbele.
(i) Siyo kukosa rasilimali kunakofanya watu wafeli, bali ni kukosa maono.
Mahitaji huwa yanafuata baada ya maono. Kama maono yako ni madogo huwezi kupata mahitaji makubwa. Mahitaji na maono huwa yanaenda pamoja.
Miaka mingi nyuma huko kuna mtu alikuwa na Mawazo ya kutengeneza, ndege, serikali ya Marekani, ikampa sapoti kubwa sana. Alipewa kiasi cha USD 50,000. Fedha nyingi sana kwa wakati huo. Ila inawezekana maono hayakuwa sahihi licha ya financial resources alizopewa.
Ila mwanzoni mwa miaka ya 1900’s Wright brothers, walikuja kugundua ndege wakiwa na resources ndogo zaidi kama USD 2,000. Hawa ndio wagunduzi wa kwanza wanaojulikana kama walioanza kurusha ndege. Misconception ya kwanza ya kuiondoa ni kuwa fedha ni tatizo.
(ii) Siyo kile kiwango cha watu wanaokupinga kinachokurudisha nyuma.
Ni kiwango chako cha maono. Maono yanatengeneza persistent. Maono yanatengeneza perseverance, – kukomaa. Maono yanatengeneza ile hali ya kutokata tamaa.
Hata Mark Twain anasema It’s not the size of the dog in the fight, it’s the size of the fight in the dog
Unasema hili swala lazima liishe hata katika mazingira ni magumu.
(iii) Siyo kukosa connection inayofanya usipige hatua. Usiue ndoto zako sababu ya lack of connections. Watu wanashika mkono watu ambao tayari wana maono. Aliyenacho huwa anaongezewa, asiyenacho hata kile kidogo alichonacho atanyang’anywa. Maono unapokuwa nayo, huwa yanatengeneza mazingira ya kukutana na watu watakaokushika mkono, Badala ya kuangalia nini kinatokea nje, jitahidi kuangalia maono yako, na uyafanyie kazi. Fikiria unataka kufika wapi, halafu jenga picha ya ndani.
Naendelea Kujifunza: Tujifunze Pamoja
Follow CantonaCast Television
YouTube https://youtu.be/JdAyEBqhCIQ
Yatimize maono Yako
#TheHeartBeatofAfrica
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.