Baraka za kufanya mambo mema!

Tunatakiwa kuendelea kutenda mema bila kuvunjika moyo, maana tutakuja kulipwa mema. Tunaishi kwenye duniani, ambayo tumefikia sehemu tunalipa uovu kwa uovu. Tunafanya mambo mabaya, na wakati mwingine wala hatia haipo. Ukishakuwa kwenye dunia ya aina hii, lazima uichunguze dhamira yako, maana itaendelea kuharibika.

Ili uwe mtu ambaye unapata matokeo makubwa lazima ujifunze kutenda mema.
Ukifanya mambo mema yanaweza kubadilisha

Maisha ya wengine, na wewe unapata baraka.

  1. Kuna uwezekano wa kuchoka, kwa kutenda mema.

Kufanya mema kuna wakati inapunguza energy. Inapunguza nguvu. Na kuna wakati inapunguza hamasa. Unapomsaidia mtu kwenye fedha, au kutoa muda wako, unatumia nishati.

Si jambo la ajabu sana kujisikia uchovu. Kutenda mema siyo jambo jepesi, inahitaji kujituma, inabidi kuvumilia. Lazima ifike mahali ukubali kuwa si jambo rahisi. Maana kuna wakti utakuwa unafanya pekee yako na hakuna mrejesho Chanya.

Si jambo rahisi. Doing good is not an easy thing. Usichoke, usiishiwe nguvu. Lazima kuwe na dhamira ya makusudi. Na hata ukichoka, usikate tamaa. Unawekeza.

  1. Kila jambo jema, ni mbegu kwa ajili ya kesho.

Unapotenda mema, haufanyi tu jambo ambalo litapita. Chochote unachofanya sasa hivi ni mbegu unayopanda kwa ajili ya kizazi chako.

Kila mbegu inakuja kulipa baada ya muda Fulani. Si kila wakati utatenda mema leo, halafu utavuna mema leo leo. Ila amini tu, hakuna mbegu itakayopotea.

Hata mkulima anajua, ukipanda mbegu leo, anajua kabisa atakuja kuvuna baada ya muda Fulani kupita.

  1. Kutakuwa kuna muda wa kuja kuvuna.

Mema yatavunwa tu kwa wakati wake. Na ubaya pia una mavuno yake. Kuna wakati unaweza hata mavuno usiyapate wewe, wanaweza kuja hata kuvuna Watoto wako, au wajukuu wako.

Sisi ni wajukuu na wajukuu wa kizazi cha Abrahamu, lakini mpaka leo, tunavuna baraka kupitia kwa Abrahamu. Na uzuri wa mbegu, zinakuwa chache sana, lakini mavuno au matunda yanakuwa ni mengi sana. Punje moja ya mhindi, inazaa mahindi mengi.

Hakuna anayepanda mbegu, akavuna kiasi cha mbegu. Mbegu unayopanda ujanani, ndio utavuna ukubwani.

  1. Kuna uwezekano wa kugeuka.

Kuna watu wamejeruhiwa, mpaka wanafika mahali wanageuka. Walifanya mema, ila wakasalitiwa. Hawa watu wanaweza kugeuka. Unatakiwa kujua mavuno ni kwa wale watu watakaofanya kwa muendelezo.

Pale ambapo, hakuna mtu wa kukusifia, lakini unaendelea kutenda mema. Endelea kutenda mema, sababu siyo yule unayemtendea wema ndio lazima akulipe. Mungu atakulipa kupitia mtu tofauti kabisa.

Na siyo lazima ulipwe wewe, anaweza kuja kulipwa hata mtoto wako. Unatakiwa kujua tu, kuna baraka katika kutenda mema. Anza kutenda mema leo kwa mtu, mtu usiyemjua kabisa.

Yatimize maono yako

#TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment