Rais Biden na Donald Trump kushinda kinyang’anyiro cha uteuzi wa vyama.

Rais Joe Biden na Donald Trump kila mmoja anakadiriwa kuwa ameshinda katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa vyama vyao katika majimbo kadhaa usiku wa kuamkia leo. Hiyo inatokana na taarifa kutoka kwa mtandao washirika wa BBC nchini Marekani, CBS News.

Wote wawili watatunukiwa wajumbe. Kadiri wanavyopata wajumbe wengi zaidi, ndivyo kila mshindani anavyokaribia kupata kibali rasmi kutoka kwa chama chao ili kuwania uchaguzi wa urais baadaye mwakani.

Kwa Democtrats :
Biden hadi sasa anatarajiwa kushinda katika kinyang’anyiro cha uteuzi katika majimbo 11 ambayo yalipiga kura Jumanne: Alabama, Arkansas, Colorado, Maine, Massachusetts, North Carolina, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont na Virginia.
Pia amethibitishwa usiku wa kuamkia leo na chama chake kuwa ameshinda jimbo la 12 , Iowa, ambapo watu wameweza kupiga kura katika kikao kwa njia ya posta tangu Januari.

Kwa Republican :

·Trump hadi sasa anatarajiwa na CBS inasema kuwa ameshinda mashindano ya uteuzi katika majimbo tisa : Alabama, Arkansas, Colorado, Maine, North Carolina, Oklahoma, Tennessee, Texas na Virginia.
Jimbo moja – Massachusetts – limeainishwa kama “linalompendelea” Trump

Unaweza pia kusoma:

Je ‘Super Tuesday’ ni nini na kwanini ni muhimu?

#TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment