Mambo 3 makubwa usiyoyajua kuhusu kukataliwa…

Mtu mmoja aliwahi kusema…

“Everytime I look back I realize that the times when I thought I was being rejected from something good…

…I was actually being directed to something better”.

(Kila wakati nilipofikiria kuwa nakataliwa na ninakosa kitu kizuri kumbe…

…ilikuwa njia ya kunisaidia ili nipate kitu kikubwa zaidi kwenye maisha yangu).

Unaweza kupitia “REJECTION” kwenye kazi, kwenye biashara, mahusiano ama hata siasa.

Kuna mara nyingi tukikosa tunachokitaka huwa tunapitia maumivu makali sana…

…kwani tunaamini ndio ilikuwa njia yetu ya kufanikiwa.

Kuna mambo muhimu unatakiwa kuyafahamu kuhusu KUKATALIWA:

  1. Kuna Watu / Kitu Mungu Anakuepusha Nacho.

Hata kama angekuambia sasa hivi kutokana na uhitaji wako ulivyo mkubwa usingeelewa.

Njia rahisi anayotumia ni kufanya wakukatae ili USIKOSE KIKUBWA kilichoandaliwa mbele yako.

Ni sawa na kusema wanaokukataa wametumwa na Mungu wafanye hivyo bila hata wenyewe kujua.

Baadaye utaelewa na kushukuru kuwa walikukataa.

Kuna BALAA na MAJUTO wanakuepusha nayo.

  1. Kuna Watu Wanakukataa Kwa sababu Hawajaelewa Kabisa ULICHONACHO.

Yaani ni kama dhahabu iliyotupwa zizi la ng’ombe, itakanyagwa hovyohovyo.

Ukikataliwa na bosi wako akasema hauna thamani…

…usikubali ikuingie moyoni.

Ni kwamba hajaijua thamani yako.

Haujawahi kuona timu moja inamuacha mchezaji kwa kusema hafai…

…na anachukuliwa na timu nyingine kwa bei ghali tena anakuwa wa kutumainiwa?

Usiruhusu ambao bado hawajaijua thamani yako kukufanya ujione hauna thamani.

  1. Kuna Watu Wanakukataa Ikiwa Ni Njia Ya Kukusaidia Kufanya Maamuzi Sahihi Kuhusu Maisha Yako.

Mara nyingi kuna wakati mihemko inaongoza maamuzi ya wengi.

Ukikataliwa unaanza kutafakari kuhusu mambo mengi…

…na hapa ndipo unaposaidika kufanya maamuzi sahihi.

Kwa vyovyote vile WALIOKUKATAA na WANAOKUKATAA watashangaa UTAKAVYOFANIKIWA…

…kama HAUTAZIMIA MOYO.

Kama umejifunza kitu kupitia ujumbe huu comment neno “SITAZIMIA MOYO”

Yatimize Maono Yako

#TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment