Hofu ya kuwa mbali na unapwapenda!!!

Hofu kubwa ambayo kila mtu anayo kwenye maisha ni…

…kupoteza au kuwa mbali na watu tuliowazoea sana.

Hata hivyo, katika safari yako kuelekea juu kuna wakati…

…utalazimika kukubali kupoteza baadhi ya watu.

Hii haisababishwi na chuki au ugomvi…

…ila kuna wakati inabidi tu.

Kuna watu wanaweza kuambatana na wewe…

…ili mradi tu uko chini yao.

Ukianza tu kuinuka inalazimika wakae mbali na wewe…

…la sivyo watageuka kuwa mwiba.

Kuna watu ambao wakiendelea kuwa karibu sana wanaanza…

…kutumia kukujua kwako na madhaifu yako kama silaha ya kukuangusha.

Kuna watu ambao utakapoanza kujiamini na kupambania…

…ndoto yako kubwa watakugeuza kuwa adui.

Yaani watu hawa, kama utaendelea kuwa mtu wa kawaida basi…

…hawana shida kabisa.

Ila utakapoanza tu kupambania ndoto zako kubwa wataanza kuchukia.

Wako tayari wakae na wewe na wakusapoti ukikubali na kuridhia kuendelea kuwa mdogo…

…ila ukianza kujaribu kuwa mkubwa tu, wanakugeuza adui.

Muda ukifika wa kuachana na watu sio lazima iwe ugomvi…

…achana nao kwa amani.

Usiogope ni sehemu muhimu ya kukua kwako.

Tafadhali ukimaliza kusoma nisaidie kushare..

Yatimize Maono Yako


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment