Uganda: Wakili wa Besigye ashtakiwa kwa kosa linalohusiana na uhaini

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph June 18, 2026 15:00 (EAT)

Meya wa zamani wa Uganda na wakili wa kiongozi wa upinzani anayezuiliwa nchini Kizza Besigye kwa tuhuma za uhaini pia ameshtakiwa kwa kosa linalohusiana na uhaini.

Erias Lukwago alifikishwa mbele ya mahakama ya hakimu mkazi mji katika mkuu Kampala akionekana kuwa dhaifu, vyombo vya habari vya ndani viliripoti, siku chache baada ya kukamatwa nyumbani kwake.

Amekanusha mashtaka dhidi yake na kurudishwa gerezani hadi wiki ijayo kesi yake itakaposikizwa.

Kukamatwa kwake siku ya Jumatatu kulizua shutuma baada ya mkuu wa jeshi la nchi hiyo na mwana wa rais Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kujigamba kwenye mitandao ya kijamii kuhusu tukio hilo.

Mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambaye alitoroka nchini Uganda kwa kuhofia maisha yake baada ya kugombea urais wa Januari, alidai kuwa Lukwago alikamatwa kwa amri ya Kainerugaba alipokuwa akijiandaa kuwasilisha wito wa mahakama kwa mkuu wa jeshi.

“Ninatoa wito kwa pamoja kupinga hali hii ya kutokujali sheria,” alichapisha kwenye mtandao wa X.

Familia ya Lukwago ilienda mahakamani kudai amri ya kuwalazimisha maafisa wa usalama wanaowatuhumu kumteka kufichua aliko na kumwachilia ikiwa “amekufa au yuko hai”.

Familia inasisitiza kuwa Kainerugaba alihusika na kukamatwa kwa Lukwago kwa sababu alijigamba kumdhulumu kwenye mitandao ya kijamii.

Uswizi: Wajumbe wa Iran, Marekani kukutana kesho kwa mazungumzo na wapatanishi

.

Uswizi ambayo ni mwenyeji rasmi wa mazungumzo ya makubaliano ya kumaliza vita kati ya Iran na Marekani imesema kuwa imejiandaa kwa mkutano kati ya wajumbe hao.

“Mpango uliofikiwa ni ni kwamba wajumbe wa Marekani na Iran, pamoja na wawakilishi wa Pakistan na Qatar kama wapatanishi na nchi nyingine zenye nia, watakutana kesho mjini Bergen kwa majadiliano ya awali juu ya utekelezaji wa makubaliano,” ilisema nchi hiyo katika taarifa.

Taarifa hiyo pia imearifu kwamba, “Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu muda na maelezo ya mkutano huo.”

Iran kuzitoza ada meli zinazopita kwenye Mlango wa bahari wa Hormuz

.

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema katika mahojiano yaliyopeperushwa kwenye televisheni ya taifa ya nchi hiyo kwamba Mlango wa bahari wa Hormuz “hautarejea katika hali ya kabla ya vita.”

Ameongeza kuwa: “Iran ina haki ya kusimamia Mlango-Bahari wa Hormuz na, bila shaka, tutatoza ada kwa huduma hizo.”

Nchi hiyo sasa itatoza meli zinazopitia njia hii muhimu ya baharini baada ya siku 60.

Maelewano ambayo Trump alitia saini yalisema kwamba katika muda mrefu, Iran itashirikiana na Oman na mataifa mengine ya Ghuba kuunda makubaliano “ya kina” juu ya jinsi ya kusimamia Mlango-Bahari wa Hormuz.

Marekani inaamini kuwa Iran itadai haki zake “kichokozi”, lakini mataifa ya Ghuba “hayatakubali” siku zijazo ambapo kuna mfumo wa kodi, afisa mmoja alisema.

Milio ya risasi yasikika katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Niger

Milipuko na milio ya risasi imesikika ikitokea uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Niger, Niamey, wakazi wameiambia BBC.

“Nilisikia milio ya kwanza ya risasi saa 06:00 (05:00 kwa saa za hapa) nilipokuwa msikitini. Lakini hali sasa imedhibitiwa,” mtu mmoja alisema.

Milio ya risasi iliodumu kwa saa mbili, ilitoka kwenye mlango wa kuingia uwanja wa ndege, aliyeshuhudia aliambia shirika la habari la AFP.

Niger imekuwa ikipambana na uasi wa wanamgambo wa Kiislamu kwa muongo mmoja na mwezi Januari washukiwa wa jihadi walianzisha shambulio kwenye uwanja huo wa ndege.

Kama majirani zake, Burkina Faso na Mali, Niger inaongozwa na kikosi cha kijeshi ambacho kiliingia madarakani kwa sababu ya serikali kushindwa kushughulikia vurugu.

Wakazi wameiambia BBC kwamba shambulio la Alhamisi lilizuiwa na jeshi, ambalo sasa linawasaka washambuliaji waliokimbia ambao inasemekana waliacha silaha zao.

Mamlaka bado haijatoa maoni na hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo. Lakini mshirika mmoja wa kundi la Islamic State alisema ndilo lililofanya shambulio la Januari.

Mama yake Vozinha awasili Praia kabla ya safari ya Marekani

Mama yake kipa mkongwe wa Cape Verde Vozinha amewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Praia kujiandaa kwa safari yake ya kuelekea Marekani.

Ana Cândida Évora aliondoka katika mji wake wa São Vicente Jumatano usiku, akiandamana na mbunge anayewakilisha wilaya yake.

BBC inafahamu kuwa Bi Évora anaweza kuwasili Marekani kati ya Ijumaa na Jumamosi, kabla ya mchuano wa Jumapili kati ya Cape Verde na Uruguay huko Miami.

“Nina furaha,” aliiambia BBC, akionyesha matumaini kwamba kila kitu kitaenda sawa.

“Ninabeba ujasiri wa kipekee kwa raia wa Cape Verde walioko huko. Tutapambana na kung’ara kwenye uwanja huo,” aliongeza.

Kwenye uwanja wa ndege wa São Vicente, aliwakumbatia wanafamilia na wapendwa wake kabla ya kuelekea Praia.

Utafiti waonesha mafanikio makubwa ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi

.

Takriban maisha ya watu 200 yameokolewa nchini Uingereza kufikia sasa kutokana na chanjo inayokinga saratani ya shingo ya kizazi, hii ikiwa ni kulingana na uchambuzi uliochapishwa katika jarida la la Lancet.

Utafiti huo wa kwanza wa aina yake umeonyesha kwamba vifo vimepungua sana tangu wasichana wenye umri wa kwenda shule walipopewa chanjo ya human papillomavirus (HPV) mwaka 2008.

Ripoti ya utafiti huo inaonesha kuwa kati ya 2020 na 2024, hakuna vifo vya saratani ya shingo ya kizazi vilirekodiwa kwa wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 – mara ya kwanza kutokea kwa kipindi cha miaka mitano.

Bila chanjo, takribani vifo ishirini na vitatu vingetarajiwa.

Prof Peter Sasieni, mtafiti mkuu katika Chuo Kikuu cha Queen Mary cha London amesema:

“Inashangaza kufikiria kwamba chanjo inaweza kukaribia kumaliza aina fulani ya saratani,”

Utafiti huo pia uligundua kuwa watoto hao waliochanjwa wakiwa na umri wa miaka 12 au 13 sasa hawakabiliwi kabisa na hatari ya kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo kabla ya umri wa miaka 30.

Kabla ya kampeni ya chanjo ya HPV, takribani vifo 20 kila mwaka vilikuwa vikirekodiwa katika kundi hilo la umri.

Kwa ujumla, saratani ya shingo ya kizazi bado ni saratani ya 14 kati ya wanawake nchini Uingereza, na watu 3,300 hugunduliwa kila mwaka.

Inafikiriwa kuwa HPV, virusi ambavyo huenezwa kwa mgusano wa karibu wa ngozi kwa ngozi, husababisha asilimia 99 ya maaambukizi yote ya saratani hiyo.

Maambukizi mengi ya HPV hupita bila matatizo yoyote, lakini mengine husababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida ya seli na yanaweza kusababisha saratani miaka mingi baadaye.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,431 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply