Usilazimishe kwa kila ubishi!!!

Moja ya HEKIMA muhimu kwenye maisha ni kujua kuwa, HAUTAKIWI kulazimisha kwenye kila MABISHANO na KUTOFAUTIANA.

Uwe mtu wa kupima mambo, kuna wakati unaweza kupata USHINDI kwenye jambo moja ila ukawa UMESHINDWA kwenye mambo MENGINE MENGI SANA.

Kuna wakati, AMUA KUMALIZA UGOMVI kwa kukubali KUSHINDWA ili UTUNZE AMANI yako.

Kuna wakati AMANI yako ni muhimu kuliko KUSHINDA HOJA.

Usisahau kuwa, kuna watu wakilazimisha kushinda ila WAKAPOTEZA MAHUSIANO.

Usijali utaonekanaje, kama ukipima ushindi unaotafutwa, hautakudhuru UKIMPATIA, basi amua kumpatia.

UBAKIE na AMANI yako, UWAPE USHINDI WAO.

Sio kila wakati unapowapa ushindi inamaana UMESHINDWA, kuna wakati UMESHINDA kwa namna ambayo wao HAWAIJUI.

Yatimize Maono Yako


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment