Maalum Kwa Wale Ambao Wameshawahi Kusaidiwa Maishani…
Kuna watu wengi sana wanapitia MAGUMU na MAZITO ila hawawezi kukuambia au kuyaweka wazi.
Kuna wengi ambao kiwango cha MAUMIVU wanayoyapitia HAYAWEZI kuelezeka…
…ingawa kwa nje ukiwaona bado WAMEVAA vizuri na wengine WANATABASAMU.
Kuna wengi ambao wewe unawaona ni tumaini lako…
…ila siku wakikuambia yanayowasibu utatamani UANZE kuwatia MOYO.
Kuna wengine WAMEBEBA MIZIGO mizito NDANI yao…
…ila bado ukiwaomba MSAADA na MUDA wao wanakusikiliza na wanakusaidia.
Kuna wengi ambao tangu waanze kupitia magumu…
…hawajawahi kutiwa moyo na mtu yeyote katika familia, ofisi au marafiki zao.
Ingawa wao wamekuwa mstari wa mbele KUSIMAMA kwa ajili ya wengine…
…ila wao HUWA WANAACHWA PEKE YAO.
Watu huamini kuwa hawakutani na matatizo…
Au wakikutana nayo basi wana uwezo wa KUYATATUA WENYEWE bila KUHITAJI MSAADA WA MTU.
Leo, ONGEZA TUMAINI kwa mtu.
Badala ya KUMLAUMU tu, KULALAMIKA tu au KUSEMA HAKUJALI.
Tumia njia tofauti, Onyesha kuwa UNAMJALI.
Muulize ANAENDELEAJE, Mshukuru kwa BIDII anayofanya…
…MTIE Moyo kwa Moyo wake wa UKARIMU n.k
Kuna mtu anasubiri NENO LAKO LEO…
…ili AVUKE kwenye CHANGAMOTO inayokaribia KUMKATISHA TAMAA.
Mthibitishie kuwa HAYUKO PEKE YAKE.
KUMBUKA: Hata wanaoonekana wana NGUVU kuna wakati HUITAJI MSAADA PIA.
Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA”
Yatimize Maono Yako
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.