Kubali kuchekwa….

Maalum Kwa Wanaoogopa Kuchekwa…

Ukifanya na USIPOFANIKIWA utachekwa…

Ukijaribu kuanza na UKAFELI utachekwa…

Usipofanya ukabakia ULIPO utachekwa…

Wengine watakucheka kwa kujaribu UJANANI kwa sababu ulifeli…

Wengine watakucheka ukiwa MZEE kwa sababu haukujaribu ukiwa Kijana…

Yaani, inabidi tu uamue uchekwe WAKATI GANI…

Unachotakiwa kukumbuka ni kuwa, bila kujali umefeli mara ngapi…

…kila unaposhifeli kuna kitu UTAJIFUNZA.

Utakaporudia tena kufanya, hautaanza Kama zamani.

Kuna NDOTO nyingi sana na MAWAZO mengi sana yamepotea…

…kwa sababu ya watu kuogopwa kuchekwa.

Kuna wengi wenye uwezo mkubwa ila kwa sababu ya kuogopa kuchekwa…

…hawajaanza hadi leo.

Nikukumbushe kuwa, watu wa kukucheka kila siku WANAIBUKA WAPYA.

Amua uchekwe sasa hivi kwa KUJARIBU…

…au uchekwe Baadaye kwa KUTOJARIBU.

Leo, fumba macho achana na wanaokucheka…

…chukua hatua kuhusiana na malengo yako.

Kama umejifunza kitu comment neno “NIMEJIFUNZA.

Yatimize Maono Yako


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment