____Hawa ni wale watu ambao waliwahi KUKATALIWA huko nyuma.
Wengine waliwahi kukataliwa na WAZAZI wao wakiwa wadogo….
…na yamkini hadi leo hawamjui BABA YAO.
Wengine ni wale ambao waliwahi kukataliwa/kusalitiwa na WAPENZI wao huko nyuma.
Yaani hawa hadi leo wana kidonda ambacho bado HAWAJAPONA.
Halafu kuna wale ambao waliwahi kukataliwa/kufukuzwa na bosi wao.
Hali hii imewapelekea kujiuliza maswali KILA SIKU.
Watu wa namna hii huwa wanakuwa na changamoto sana kwenye KUPENDWA.
Yaani ukiwa na mtu wa namna hii…
…inabidi UTUMIE NGUVU sana kumthibitishia kuwa UNAMPENDA.
Mengi utakayofanya atakuwa anatia SHAKA…
…hata pale utakapokuwa UMEJITAHIDI kufanya bado atakuwa mtu ambaye HARIDHIKI.
Kiufupi, jiandae kukabiliana na changamoto ya…
…KUTUMIA NGUVU NYINGI sana kumpenda mtu wa NAMNA HII.
Tatizo wanalokuwa ni kuwa mara nyingi hata kwenye mahusiano huwa MGUU MMOJA NJE…
Mguu mmoja ndani na huwa HAWAFIKIRII mara mbili KUACHA na KUANZA UPYA.
Kama wewe umesumbuka sana na changamoto ya KUKATALIWA huko nyuma katika maisha yako…
…kiasi kwamba hivi sasa HUAMINI mtu!
Na hata ukimuamini ni KWA MBINDE SANA…
…na unakaa naye kimashaka mashaka nashauri usome kitabu changu cha…
“Maumivu Ya Moyo, Jinsi Ya Kupona Na Kuyatumia Kwa Faida”.
Kitakusaidia sana kuweza kupona Maumivu uliyopitia siku za nyuma na uanze kuishi kwa furaha.
Pia nashauri usome kitabu changu cha Lugha 5 Za Upendo…
…Hiki kitakusaidia sana kuboresha mahusiano yako na mpenzi wako.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.