Mungu alimuumbia kila mtu hazina ya kipekee ambayo kwa hiyo anaweza kuyafurahia maisha yake hapa duniani.
____Hazina hiyo haihitaji kuwa na fedha ili uweze kuipata ila inahitaji ujitambue ili uweze kujua.
Hii ndio tunaita maono.
Maono ni picha aliyonayo mtu juu ya maisha yake anayoyataka.
Ni ramani inayokudadavua wewe ni nani.
Ni dira inayoongoza maisha ya mtu.
Mwenye hekima mmoja aliwahi kusema huwezi kukiishi kile ambacho hujawahi kukiona…
…iwe kwavmacho haya ya nyama au kwa macho ya ufahamu.
Kile unachokiona kwenye moyo wako ndicho kinachoamua maisha yako.
Maisha yanaanza pale unapoanza kutengenezavmaono ya maisha yako.
Hii inamaanisha maana ya maisha imefungwa kwenye maono.
Asiye na maono hana maisha.
Kumbuka sio kila mwenye uhai ana maisha.
Ili uweze kuyaishi maono yako huna budi kukubali kupitia mchakato wa maono yako.
Maana maono ndiyo yanaamua kila kitu kwenye maisha yako.
Asiyevna maono hana kiasi, hana sababu inayomfanya aishi wala tumaini la maisha.
Usikubali kufa kabla ya kuyaishi maono yako.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.