Kila mtu ana njia yake kuonyesha maumivu

Kila mtu ana NJIA YAKE ya kuonesha MAUMIVU.

Kuna wengine wakiwa kwenye maumivu huwa WANAKAA KIMYA kabisa hawataki kuongea na mtu.

Yaani, huwa wanajitenga na hawataki kuwasiliana na mtu.

Wapo wengine ambao wanaonesha WAZIWAZI.

Yaani wakiwa na maumivu utawaona tu.

WATALIA kwa machozi au watatoa SAUTI utakayosikia.

Wengine wakiwa na maumivu wataongea kuanzia Asubuhi hadi Jioni.

Yaani wanarudia jambo hilohilo kila saa na wanamsimulia kila mtu.

Halafu kuna wale ambao wao wakiumia tu, watakimbilia kupost kwenye mitandao.

Ataanza WhatsApp Status, Facebook, Instagram n.k

Jijue wewe kwanza na wajue wengine wanafanyaje.

Tunatofautiana namna ya kukabiliana na maumivu.

Heshimu namna ya mwingine kuonesha maumivu yake.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment