Unapokumbana na Magumu

Kuna wakati utapitia nyakati NGUMU na zenye MAUMIVU na itaonekana kama vile MSAADA unaouhitaji UNACHELEWA.

Mara nyingi, tukipita nyakati kama hizi tunaingiwa na hali ya KULAUMU na KULALAMIKA.

Usisahau kuwa, nyakati za namna hii huwa zina kazi muhimu mbili katika maisha yako.

1. Kazi ya kwanza ni kukusaidia KUJENGA MISULI muhimu kwenye maisha yako.

Kumbuka hauwezi kuwa IMARA bila kupitia mambo yanayokulazimisha kuwa imara.

Ukiona MAMBO unayoyapitia HAYAONDOI uhai wako ujue yamekuja kukuimarisha na kukuandaa na yajayo.

Usikubali KUZIMIA moyo, pambana USHINDE.

Kazi ya PILI ni kukusaidia KUCHUJA WATU kwenye maisha yako.

Ni kipindi cha namna hii ndio utajua marafiki HALISI na wale wasio wa kweli kwenye maisha yako.

Nakuombea UVUKE SALAMA kwa USHINDI.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment