Tunza Siri

UKIAMINIWA kupewa taarifa za ndani na MTU, usizitumie KUMNYANYASA.

Kuna watu wengi sana wameumizwa kwa sababu WALIJIFUNUA kwa watu ambao baadaye WALIGEUKA kuwa ndio chanzo cha MAUMIVU YAO.

Yaani, mtu aliwaamini kwa kiwango cha kuwapa taarifa zao za NDANI na za SIRI.

au wengine WALIAMUA kuwaweka KARIBU na wakafahamu mambo YALIYOJIFICHA ambayo wengine hawayajui.

Baada ya kutofautiana au kugombana, wakaamua kutumia taarifa hizo kama sehemu ya KUWATESA na KUWANYANYASA.

Usisahau kuwa UKIAMINIWA na MTU ina maana amekupa THAMANI.

Usimrudishie MAUMIVU bila kujali kama hamko karibu tena ama la.

Usisahau kama ilivyo kwa wema, UBAYA pia ni MBEGU.

Ukiipanda kuna siku UTAIVUNA PIA.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment