Jinsi ya kuwa mtu mwene aman moyoni

Jinsi Ya Kuwa Mtu Mwenye Amani Moyoni. Njia mojawapo ya kujihakikishia unakuwa mtu mwenye amani moyoni ni kuwa mtu unayesamahe wanaokukosea.

Jonathan Lockwood aliwahi kusema…

…“Wasamehe wengine sio kwa sababu wanastahili bali kwa sababu wewe unastaili amani”

(Forgive others not because they deserve it but because you deserve peace).

Kuna watu wengi wanaishi katika vifungo vya uchungu na kutokusamehe.

Wengine hata wameapa kabisa…

…“huyu sitamsamehe kamwe”.

Mara nyingi tunafikiri kutokusamehe huleta madhara kwa yule asiyesamehewa…

…lakini ukweli ni kuwa asiyesamehe ndiye anateseka zaidi.

Na wakati mwingine huweza kuleta magonjwa ya moyo kabisa.

Kusamehe SIO JAMBO RAHISI ila ni la MUHIMU sana katika maisha.

Kusamehe ni kuachilia mtu uliyemshikilia katika moyo wako.

Ni kusema kuwa “Najua alifanya makusudi, hajali kama amenikosea, ameniletea maumivu na hasara ila nimeamua kumsamehe”.

Mara utakapofanya hivi utashangaa amani ya moyo inaanza kurudi na milango ya baraka inaanza kufunguka.

Kumbuka kwa kanuni ya kiroho ni kuwa “Msipowasamehe wengine makosa yenu, nanyi baba yenu wa mbinguni hatawasamehe”.

Hivi kama Mungu asipokusamehe makosa yako hadi yale umefanya sirini na hakuna mtu anajua, UTAWEZA KUFANIKIWA KWELI?

Usiwasamehe kwa sababu wanastahili, wasamehe kwa sababu wewe unastahili AMANI.

Inawezekana ni baba aliyekukataa, ni mwenza aliyekusaliti, ni rafiki aliyetumia kukujua kwako kukudhuru, ni mtu wa kazini aliyekusingizia na kukusababishia matatizo, ni mtoto wako n.k

SAMEHE.

MILANGO MIKUBWA YA MAFANIKIO unayoitafuta imefichwa kwenye UTAYARI WAKO wa kusamehe.

Anza leo, fanya sasa hivi, usisubiri muda upite.

Hata kama haujisikii, mwambie “Nimekusamehe”, tamka kwa sauti “Huyu (jina lake) nimemsamehe”

– Kisha mtafute muambie.

Wengine watakuona MDHAIFU ila wenye NGUVU tu ndio wana uwezo wa KUSAMEHE.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment