Hatua 7 Za Kufuata Ili Upate Wateja Wengi (Effective Sales Process)
____Hatua Ya Kwanza: PROSPECTING (Formula Ya Siri Ya Kuchagua Wateja Sahihi)
Kwenye hatua hii unatakiwa kuchagua aina ya mteja unayemtaka ambaye tunamuita “Dream Client”…
… yaani nikikuuliza ni mtu wa namna gani unamlenga kama mteja wako, unatakiwa kuwa na vigezo ambavyo unavitumia kumpata huyo mteja.
Ili kufanikisha hili itabidi utengeneze sifa za mteja ambaye hasa ndiye unamlenga (Clients Profile).
Hapa lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa unamjua mteja wako vizuri ili usitumie nguvu zako kuzielekeza kwa watu ambao sio wateja.
Katika hatua hii unapaswa kutengeneza Ideal Client Profile (ICP) ya wateja wako, ambayo unakuwa unaeleza vigezo vya wateja unaowalenga.
Mfano: Umri wao, eneo wanalotokea, kipato cha chini, cha kati au cha juu, unalenga jinsia gani, bidhaa/huduma yako inalenga watu wanaofanya kazi za aina gani, kiwango cha elimu yao, maeneo wanayokaa n.k.
Hii inamaana mtu yeyote ambaye haendani na vigezo vya ICP yako, hautakiwi kutumia muda wako mwingi kumuuzia.
Zoezi:
Andika ICP ya wateja ambao unawalenga kuwauzia bidhaa / huduma yako.
1.
2.
3.
Muda wowote ukiwa tayari, kuna namna 3 kubwa ninazoweza kukusaidia.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.