Unapokuwa kwenye MAUMIVU YA MOYO ni muhimu sana kuwa…
…makini kwani ni rahisi kujikuta UNAELEKEZA hasira zako kwa wasiohusika.
Kuna watu wengi sana wakati wanapitia maumivu yaliyosababishwa na mtu mwingine na…
…wamejikuta wanahamishia HASIRA zao kwa watu wasiohusika.
Saikolojia ya maumivu huwa inasema kuwa…
…mtu akiona ameumizwa na mtu fulani basi huanza kuamini kwa ujumla (generalization) kuwa kila mtu mwingine SIO MWEMA.
Ukiwa mtu wa hivi, utapoteza watu wengi MUHIMU kwenye maisha yako.
Ukiwa mtu wa hivi utafanya watu WANAOKUPENDA kwa dhati wakae MBALI na wewe.
Usiingie kwenye ule mkumbo wa kuamini kuwa kama mtu fulani amekuumiza…
…basi unatakiwa umchukie kila anayefanana naye, hata kama hausiki katika maumivu yako ya sasa.
Jifunze kujizuia kuwachukia WASIO HUSIKA kwenye maumivu UNAYOPITIA.
Jifunze kujizuia KUTOHARIBU mahusiano na watu wengine kwa sababu ya mtu mmoja aliyekusababishia maumivu.
Jifunze kuona WEMA WA WENGINE katikati ya UBAYA WA MTU MMOJA aliyekusababishia maumivu.
Wakati mwingine, wale ambao UNAWACHUKIA kwa sababu ya MAUMIVU uliyosababishiwa na wengine…
…ndio haswa waliandaliwa WAKUSAIDIE kutoka kwenye maumivu unayoyapitia.
Kuwa Makini.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.