JINSI YA KUPENDA MWANAMKE ALIYEPITIA MACHUNGU YA MAPENZI.

1. Kuwa na uwezo wa kumsikiliza,usi muhukumu,maana amepitia machungu katika mahusiano ya mwanzo.

2. Kuwa makini na maneno makali anayozungumza,mfunzo kuzungumza maneno yanayopendeza sio ya kuhukumu na kulaani.

3. Fahamu mahitaji yake na kumtia moyo.Endelea kuomba naye.

4. Usirudie makosa ambayo mpenzi wake wa zamani alitenda,kuwaa wa utofauti.

5.Tarajia atasema katika kipindi fulani,anahisi vibaya,kutokana na kipindi cha nyuma,anatafuta mwanamme anaye mjali.

6. Mfanye kucheka na kufurahi,weka tabasamu machoni mwake.Sema naye,wakati mwingine usizungumze maneno mazito wakati mwingine kuwa mcheshi hilo linatosha.

7. Tarajia atakushuku,wakati mambo yanapokua magumu.Onyesha yanawezekana.

8. Sema naye kufahamu malengo yake/maono na ndoto zake,simama naye katika hilo.Anahitaji mtu sahihi kusimama naye katika safari yake ya mafanikio.

9. Onyesha unamtambua si tuu kwa swala la tendo la ndoa,mtazame moyoni na katika ubongo wake.

10.Wakati wote mkumbushe yeye ni malkia,onyesha ana kesho kuu,wakati anaona haliwezekani. 11. Muepushe na jana yake, simama naye leo yake na kesho yake,iwapo wapo maadui simama naye kidete kumwepusha asipokee machungu.

12. Uvumilivu naye,itachukua mda yeye kupona jiraha.

13. Usizungumze kuashiria umechoka naye.

14.Mrekebishe kwa upendo. Hili litaponya makovu.

15. Unaposimama naye,pia jirekebishe iwapo una machungu ya mahusiano yako ya zamani,maana hili litakusaidia usimkwaze.

16. Kubali awe sehemu ya maisha yako.Litamfanya kukubalika,wakati mwanamke anafahamu anapendwa anapona majeraha haraka.

17.Unaweza kuwa na mtu kwenye maisha yako anayedhani ni wamsaada sana kwako kumbe ukijitafakari hakuna anachofanya zaidi ya kupoteza muda wake na wakwako tu.

18. Nivema ujue, ufahamu na ikuingue akilini sawia kwamba kukosa sana muda wa faragha “quality time” na mke au mume wako ni kuitia ndoa yako majaribuni haswa. Najua mko bize, najua mnaitafuta pesa, lakini jua tu kwamba siku ndoa yenu ikivunjika ndio utakuwa bize zaidi na stress juu. Usije kusema sikukwambia.

19.Moja ya makosa makubwa ambayo hufanywa na wanawake wengi kwenye mahusiano na ndoa ni kutoa lawama au malalamiko kwenye kila kitu kwa wanaume wao pasipo hata kutazama vile vichache vya kushukuru, kupongeza au ku appreciate. Sio kweli kwamba mtu anafanya madhambi tu na hakuna hata jema moja ulionalo. Tabia hii imewakatisha tamaa wanaume wengi na imewafanya wengine kuwa wabaya zaidi. Usitazame mabaya tu. Hata jema lione na liseme pia.

20.Vitu viwili muhimu sana umwombe Mungu akusaidie daimaa. Akupe mwenza unayempendab. Akupe kazi unayoipendaUkikosea kimoja uta struggle tu hata kama utajitahidi kutuonyesha unatabasamu. Usifanye mchezo unatoka kwenye kazi usiyoipenda unaenda nyumbani kukutana na mke/mume usiyempenda.

Cantona School of ThoughtsTembea Youtube

Subscribe Youtube channel yangu

CantonaCast Television https://youtu.be/l-hQx4EfR_Y

Website: cantonadigital.wordpress.com

Email:cantona.online254@gmail.com

#MahusianoNaNdoa#IpoSiku

#CantonaJoseph


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment