FAHAMU UMUHIMU KUHUSU USINGIZI,TENDO LA NDOA NA MAPENZI.

1. Unapoenda kulala mwanzo usafi muhimu oga.Tendo la kumegana linahitaji usafi,usafi unavutia mpenzi wako kumegana nawe.

2. Mnapolala pamoja ni sehemu ya kudhihirisha unamjali mwenzako,mwenzako anajihisi anakubalika katika maisha yako,hili litafanya azidi kuaminia pendo lako kwake.

3.Swala ambalo linaleta mgogoro katika ndoa nyingi ni ukosefu wa uaminifu,kumegana nje ya ndoa usherati,uzinifu,mwenzako anafaa asishuku anasalitiwa penzi lenu.

4. Rejea nyumbani mapema,utakua na mda bora kushiriki chajio pamoja na maombi kabla hamjalala.Hili huondoa wasiwasi.

5. Tenga muda wa kujulia hali mwenzako,usifukuzie maisha sana,ukasahau umuhimu wa ndoa,usikimbilie kumegana pasipo maandalizi ya romance.

6. Jenga tabia ya kusema usiku mwema mpenzi wangu,asubuhi njema kichuna changu malkia/mfalme wa moyo wangu.

7. Unapovalia nguo zako wacha nguo ikadhihishe ni sehemu ipi upo na shughuli ipi mnafanya.Iwapo ni chumba cha kulala mavazi ya eneo hilo yasiwe ya kujificha maungo yako.

8. Mwandae mwenzako vizuri,fanya utaratibu kupatia full romance,mpe busu,mpapase sehemu ambazo anafurahia onyesha unahisia kali naye.

9. Kabla mke/mme wako hajalala hebu mulize hali yake ipo vipi?

10.Unapogundua mwenzako amechoka kufuatia pilkapilka za maisha,wacha apumzike ,onyesha una utu,usilazimishe tendo la ndoa mwenzako akiwa amechoka.

11. Epuka kutazama runinga sana au mda wako wote ni kutazama runinga,au upo mtandaoni mda wote.

12. Boresha hisia za mwenzako kwa kupongeza nafasi yake kwako na jinsi alivyo mrembo.

13. Usitarajie mambo yatakua sawa wakati wa kumegana,iwapo umekua haumjali mwenzako na una ujeuri fulani mambo yanaweza kuharibika kitandani.

14. Tambua mazungumzo ya pillow talk ni bora sana,pillow talk isiwe ni sehemu ya mazungumzo ya kuleta maswala ambayo sio ya makuzi ya mahaba kati yenu.Wakati wa pillow talk ni mda bora wa kulea hisia za mwenzako.

15.Mwili wako unapopata kupumzika vizuri,nyinyi wawili mtafurahia swala la kumegana vizuri na kukuza hisia za mwenzako.

16. Iwapo mna mtoto mdogo shirikiana na mwenzako katika makuzi ya mtoto,lisiwe swala la mtu mmoja.

17. Akili ilioyochoka hutatanisha katika ndoa,unahitajika kuwa na ubunifu wa kulea ndoa yako,usichoke.

18. Wakati mwingine tenga mda wa kulala siku nzima,mkiwa wawili kitandani sio mnamegana mnapumzika tuu,mkifurahia kuwa pamoja tuu.Ikiwezekana mnasoma vitabu pamoja au safiri pamoja kwa likizo la siku kadha.

19. Unapogundua kuna kuhitilafiana kimawazo na mke/mme wako na hili jambo linavuruga upendo wenu,usilaumu au kushambulia mwenzako kubadilika hili litafanya aendelee kudai hana makosa.Jambo la kufanya ni kuanda mda bora naye,kuwa mcheshi,onyesha una mjali.Maisha ni uchaguzi unachagua nini leo maana maamuzi ya leo yata amua kesho yako imesimama vipi.

Cantona School of ThoughtsTembea Youtube

Subscribe Youtube channel yangu

CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4

Website: cantonadigital.wordpress.com

Email:cantona.online254@gmail.com

#MahusianoNaNdoa#IpoSiku#marriagemathematics#FamiliaNaMalezi#MaendeleoNaMafanikio#CantonaJoseph


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment