Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupigia kura rasimu ya azimio kuhusu Mlango- Bahari wa Hormuz

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na  Cantona Joseph April 03, 2026 17:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

China, ambayo ina kura ya turufu, inapinga mpango wowote wa kutumia nguvu.

.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linatarajiwa kupigia kura rasimu ya azimio lililowasilishwa na Bahrain kuhusu kulinda meli za kibiashara ndani na karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz.

China, ambayo ina nguvu ya kura ya turufu, inapinga mpango wowote wa kutumia nguvu.

Bei ya mafuta imepanda kwa kasi tangu Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran mwishoni mwa mwezi Februari, na hivyo kuzua mzozo ambao sasa umedumu kwa zaidi ya mwezi mmoja na kusababishwa kuufungwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz.

Wanadiplomasia walisema Bahrain, ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama lenye wanachama 15, imekamilisha rasimu ya azimio lililoonekana na Reuters linaloidhinisha matumizi ya “njia zote muhimu za kujihami” kulinda meli za kibiashara.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain Abdullatif bin Rashid Al Zayani ameliambia baraza hilo, “Tunatazamia kupata msimamo mmoja kutoka kwa baraza hili tukufu wakati wa upigaji kura utakaofanyika kesho(Ijumaa), kuhusu rasimu ya azimio hilo” Mungu akipenda.

Hapo awali Bahrain ilikuwa imeondoa pendekezo la utekelezaji wa sheria katika jaribio la kuzuia pingamizi kutoka kwa nchi zingine, haswa Urusi na China.

Rasimu ya azimio inaidhinisha kuchukuliwa kwa hatua hizi “kwa muda wa angalau miezi sita … na hadi Baraza litakapoamua vinginevyo.”

Hata hivyo, Fu Cong, mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa, aliweka wazi katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama kwamba Beijing inapinga kuidhinisha nchi wanachama kutumia nguvu.

Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth amemtaka Mkuu wa Majeshi kuachia ngazi

Randy George
Maelezo ya picha,Mkuu wa Jeshi la Marekani Randy George

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amemtaka Mkuu wa Majeshi Randy George kuachia wadhifa wake, kulingana na CBS News, mshirika wa habari BBC wa Marekani.

Msemaji Mkuu wa Pentagon Sean Parnell alisema katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii kwamba George “atastaafu kutoka wadhifa wake kama Mkuu wa 41 wa Wanajeshi mara moja”.

Mkuu wa Jeshi kawaida huhudumu kwa kipindi cha miaka minne.

George, afisa wa kijeshi ambaye alihitimu kutoka chuo cha kijeshi cha West Point, aliteuliwa kwa jukumu hilo mnamo 2023 na Rais wa zamani Joe Biden.

Mabadiliko ya hivi punde yanakuja baada ya Trump kusema katika hotuba yake kwa taifa kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vinatarajiwa kumalizika “hivi karibuni”.

George aliwahi kuwa afisa wa jeshi katika Vita vya kwanza vya Ghuba na katika migogoro ya hivi majuzi nchini Iraq na Afghanistan.

Haijabainika kwa nini alitakiwa kuondoka. “Tunashukuru kwa utumishi wake, lakini ulikuwa wakati wa mabadiliko ya uongozi katika Jeshi,” afisa mkuu wa ulinzi ambaye hakutajwa jina aliiambia CBS.

Msemaji wa Pentagon Parnell alisema: “Idara ya Vita inashukuru kwa miongo kadhaa ya utumishi wa Jenerali George kwa taifa letu. Tunamtakia kila la heri anapostaafu.”

Nafasi yake itachukuliwa na Makamu Mkuu wa Jeshi Jenerali Christopher LaNeve ambaye atakuwa kaimu mkuu wa majeshi, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Kushambulia miundo mbinu ya raia hakutaifanya Iran kusalimu amri – Araghchi

Abbas Araghchi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kulengwa kwa daraja la B1 kwenye barabara kuu ya Tehran-Kaskazini hakutaifanya nchi hiyo kusalimu amri.

Bwana Araghchi aliandika kwenye Mtandao wa X: “Kulenga miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na madaraja ambayo ujenzi wake bado unaendelea, kamwe hakutawashinikiza Wairani kusalimu amri… Kila daraja na kila jengo litajengwa upya kwa ustadi zaidi; lakini jambo ambalo kamwe halitarekebishwa ni uharibifu unaofanywa kwa na Marekani.”

Saa kadhaa zilizopita, Donald Trump alichapisha video ya shambulio la Marekani dhidi ya daraja hilo kwenye mtandao wake wa kijamii, akiandika: “Ni wakati wa Iran kufikia makubaliano kabla ya muda kuwapa kisogo na kuiacha nchi ikiwa imesambaratika.”

Marekani yashambulia daraja kuu la Iran

.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kushambiliwa kwa daraja la B1 la Iran, iliyojengwa hivi karibuni ambayo ilikuwa inaunganisha mji wa Karaj na mji mkuu Tehran.

Trump aliongeza: “Tuliripua madaraja yao makuu matatu jana usiku. Yanaharibiwa …”

Video inaonyesha moto na moshi ukifuka juu ya daraja hilo, nasehemu ya katikati ikiwa imeachana.

Watu wanane wameripotiwa kuuawa na wengine 100 kujeruhiwa katika shambulio hilo

Daraja la B1, ambalo halikuwa halijaanza kutumika linatajwa kuwa mojawapo ya madaraja marefu zaidi katika Mashariki ya Kati. Lina urefu wa mita 1,050 na nguzo zenye urefu wa mita 136, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply