Senegal: Rais Faye anaadhimisha miaka miwili tangu kuingia madarakani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph April 02, 2026 09:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Nchini Senegal, rais Bassirou Diomaye Faye, leo anaadhimisha miaka miwili tangu aliposhika madaraka katika nchi hiyo, wakati huu akiendelea kukabiliwa na shinikiza za kutekeleza ahadi alizotoa kwa raia wa nchi hiyo.

Basirou Diomaye Faye – Rais wa Senegal AP – Olamikan Gbemiga

Rais Faye mwenye umri wa miaka 43, aliingia madarakani na kuandikisha historia ya kuwa rais mwenye umri mdogo kwenye historia ya uongozi nchini humo.

Alipigiwa kura, baada ya kuchukua nafasi ya mshirika wake wa karibu, Waziri Mkuu wa sasa Ousmane Sonko, ambaye alikuwa awe mgombea urais, lakini akazuiwa baada ya kufungwa jela.

Miaka miwili baadaye, kuna mashaka kuwa ushirikiano wake na Sonko umeanza kuyumba baada ya wawili hao kuonekana kuanza kujipanga upya kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2029, kila mmoja akijaribu kuonesha ushawishi kwenye chama tawala Pastef.

Wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa hatua ya rais Faye na Waziri Mkuu Sonko, kupambania ushawishi ndani chama hicho, unaendelea kuwagawa na kuathiri utekelezwaji wa ahadi ya maendeleo kwa wananchi wa Senegal, na ni ishara kuwa wawili hao kila mmoja anajipanga kuwania urais wa wakati wa uchaguzi ujao.

Vita vya Iran: Hotuba ya Trump yatikisa masoko huku bei ya mafuta ikipanda

Bei ya mafuta ilipanda bei na hisa kushuka soko lilipofungulia asubuhi ya Alhamisi barani Asia, kufuatia hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump, ambayo haikuhakikishia masoko ya kimataifa kwamba vita vilikuwa karibu kumalizika na kwamba usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz ungerejelea hali ya kawaida.

Mara baada ya Trump kumaliza kuzungumza, bei ya mafuta ghafi ya Brent, ambayo inatathmini kiwango cha kimataifa cha mafuta, ilipanda kwa asilimia tano hadi dola 106 kwa pipa huku masoko ya hisa barani Asia pia yalianza kudorora.

Ijapokuwa Trump alisisitiza ratiba yake ya wiki mbili hadi tatu, hakutoa hakikisho kamili kwa wawekezaji kuhusu jinsi vita hivi vitakavyoisha.

Kauli yake ya kuipiga Iran kwa mabomu na kuirejesha “kurudi Enzi za Kale” ikiwa haitafikia makubaliano imeyumbisha hali ya biashara duniani.

Hata kama mzozo huo utamalizika mwezi huu, bado itachukua muda mrefu kwa viwango vya kawaida vya usafirishaji kuanza tena kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.4 lakumba Indonesia

Tetemeko la ardhi la kiwango cha 7.4 limetokea katika Bahari ya Molucca karibu na kisiwa cha Ternate nchini Indonesia mapema Alhamisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Tetemeko hilo, ambalo lilitokea saa 06:48 kwa saa za ndani (22:48 GMT) katika kina cha kilomita 35, lilisababisha kutolewa kwa tahadhari ya tsunami ambayo sasa imeondolewa.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 70 huko Sulawesi Kaskazini alifariki baada ya kuangukiwa na vifusi vya jengo, na mtu mwingine kuvunjika mguu baada ya kuruka kutoka kwenye jengo, shirika la habari la taifa la Indonesia Antara liliripoti.

Ingawa eneo hilo hukumbwa na viwango vya juu vya mitetemeko ya ardhi, baadhi ya wakaazi wengine waliambia BBC kuwa hili lilikuwa mojawapo ya matetemeko ya ardhi yenye nguvu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

UAE inazuia makombora yaliyorushwa na Iran

Tangu kuanza kwa vita, Iran imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia katika nchi za Ghuba, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.
Maelezo ya picha,Tangu kuanza kwa vita, Iran imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia katika nchi za Ghuba, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.

Umoja wa Falme za Kiarabu imekuwa ikikabiliana na vitisho vya kushambuliwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani, wizara yake ya ulinzi ilisema muda mfupi, kabla ya hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump.

Wizara hiyo ilisema mashambulizi hayo yametoka Iran na kuwatahadharisha wananchi wake kuhusu sauti zinazosikika kote nchini wakati ikifanyashughuli ya kuzuia makombora hayo.

Katika hotuba yake kwa taifa kuhusu vita vya Iran hapo awali, Trump aliishukuru UAE na washirika wengine wa Ghuba, ambao wamekosolewa na Iran kwa kulipiza kisasi mashambulizi ya Marekani na Israel.

Trump alisema kuwa utawala wa Iran ulikuwa ukianzisha “mashambulizi ya kigaidi yaliyoharibika” dhidi ya meli za mafuta na nchi jirani ambazo “hazina uhusiano wowote na mzozo huo” alipokuwa akizungumzia wasiwasi kuhusu kupanda kwa bei ya nishati.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply