UKWELI 17 KUHUSU UAMINIFU KATIKA MAHUSIANO.

1.Uaminifu unapovunjika,mazungumzo yanakua magumu sana kuwepo. Mwanamke na mwanaume wanabuni ukuta kujitetea,kugombana na kila mmoja anavuta upamde wa kwake.

2. Usaliti wa penzi,ndicho chanzo cha kuvunja uaminifu wawili wanapopendana na kuvuruga mahusiano ya mda mrefu.

3.Unapoendelea kuchezea mwenzako,unapomdang’anya,huku ukiomba radhi huku unarudia makosa yale yale,mpenzi wako huenda akaondoa akabisa moyo wa kuamini unachosema au kutenda.

4. Chanzo cha kukosa uaminifu katika mahusiano ni ujio wa simu.Usitumie simu yako kusaliti penzi lenu.Ndio maana watu wengi wana password katika simu zao sijui wana ficha nini.

5. Iwapo unataka mpenzi wako awe na amani na maisha yake kwako,akupe mwili wake,mda wake,pesa zake,watoto huku unafichaficha simu yako kuna matatizo mahali.

6. Usitarajie mpenzi wako awe akuamini iwapo hauamini vitu muhimu.

7. Iwapo mweenyewe haujiamini,itakua vigumu sana kumwamini mwenzako,maana unafikiria mwenzako anaweza kukuacha. Lishughulikie hilo maana unaharibu

8.Iwapo utaonyesha mwenzako,wewe ni mtu usie aminika,mwenzako,ataondoa hisia zake kwako polepole,katika uhusiano wenyu au ndoa.Usivuruge uaminifu wenu.

9. Ni jambo bora kufahamu mtu anaye kufahamu zaidi ni mpenzi wako,hata pasipo kulizwa anastahili kufahamu mengi katika maisha yako.Hili linajenga uaminifu,wacha mwenzako afahamu ratiba yako ya kila siku,unachokifanya.

10. Iwapo utatumia mambo mwenzako anakufahamaisha kuhukumu mwenzako basi mwenzako atakosa imani nawe,na uaminifu utakwisha.

11.Ukosefu wa uaminifu husababisha kulemaa kwa swala la kumegana katika ndoa.Itakua vigumu kujamiana na mtu ambaye unamshuku si mwaminifu.

12. Jifunze kushiriki wazo na mwenzako linalokusumbua hata kama linakaaa ngumu,unaposhiriki unajenga uaaminifu kati yenu.

13.Uaminifu uliovunjika unaweza ukajengwa tena,iwapo aliyevunja huo uaminifu atatumia mda wake kujenga huo uaminifu.Aliyekosewa kukubali kutoshikilia jambo ambalo alikosewa.

14. Uaminifu unachukua mda,na unaweza ukabomnoa kwa sekunde moja tuu.Kwa hivyo kuwa na subira kujenga uaminifu.

15. Uwoga mkubwa ni pale unapo msamehe mtu,hauna uhakika unaye msamehe amekubali alifanya makosa,na atabadilika,au anakufanya uonekana mjinga.

16.Unapoendelea kufanya mwenzako,kujihisi salama,anakubalika,hili linalea uaminifu,uaminifu haumei kwenye bonde.

17. Katika hatua ya kujenga tena uaminifu,wacha kuliongelea swla ambalo limevunja uaminifu huo mwanzo,maana utalemaza hatua ya kukuza mahusiano yenu.

Cantona School of Thoughts

Tembea Youtube Subscribe Youtube channel yangu

CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4

Website: cantonadigital.wordpress.com

Email:cantona.online254@cantonajoseph

#MahusianoNaNdoa #IpoSiku #marriagemathematics #FamiliaNaMalezi #MaendeleoNaMafanikio #CantonaJoseph


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment