
Wanaume…………
1.Watafute marafiki wanaume watakao kukosoa wakati unapochukua mkondo usio mzuri,sio wale wanaume ambao watakuona ukiteleza maishani na wasalia kimya tuu.
2. Watafute marafiki watakao heshimu mwanamke unaye mpenda,sio wale wanaokushauri kumdhulumu kichuna chako,na kumchukulia kikawaida tuu.
3. Watafute wanaume marafiki wanaowashauri watoto wako,sio wasio na maadili mema.
4. Watafute marafiki wanaume watakao kushauri kuekeza wala sio wanao haribu fedha kwa anasa.
5.Watafute marafiki watakao acha alama maishani sio wanaofikiria kutengeneza fedha alafu wanatumia vibaya.
6. Watafute marafiki watakaodhamini familia yako na kuelewa familia yako na watakaokuruhusu kurudi nyumbani mapema kwa familia yako,sio wanakuelekeza kutorudi nyumbani mapema.
7. Watafute marafiki wa dhati utakao wamini sio watakao kuacha ukiwa katika matatizo.
8. Watafute marafiki wanaume watakaokuonya usipo jali mke wako,sio wanaokushauri kumpiga mke wako.
9. Watafute marafiki wanaume ambao watakuelekeza kwa kufahamisha ukweli mtupu kama ndugu wa karibu,sio wanaokusifia kwa maslahi yao tuu hata wakati unakumbana na magumu.
10.Watafute wanaume walio na maono,na mtazamo chanya watakao kunoa na sio watakaovuruga malengo yako.
11.Watafute marafiki wanaume wanaozungumzia mipango ya maisha na walio na utu,wanapoomba nawe sio wanaochukua mda wote kuomba nawe,sio wanaozungumza wakati wote maswala ya michezo na kucheza kamari.
12. Watafute wanaume ambao watakushauri,kuwaheshimu wanawake,sio wale watakao kushauri kuwatumia wanawake kama chombo cha kujamiana tuu.
13.Watafute marafiki wa kiume wataokupa suluhisho,sio wanaozamia sana katika mazungumzo yanayolenga siasa.
KWA WANAWAKE…
1. Watafute marafiki wanawake watakaokutia moyo,sio wambea.
2. Watafute marafiki wanawake wanaokuheshimu na kuheshimu ndoa yako,sio wanaokuvunja moyo kwa kupenda mme wako.
3. Wapende marafiki watakaokuonya sio watakaokuunga mkono uendelee kulalamika.
4. Watafute marafiki utakaopokea ushauri katika makuzi ya watoto wako,unapopata dharula.
5. Watafute marafiki ambao watachangia ukuaji wako,huku ukipata amani,sio wale ambao wataleta matatizo katika maisha yako
6.Watafute marafiki wanawake ambao watakaokushauri,kama dada sio wanao kupotosha.
7. Watafute wanawake marafii ambao unaweza kuekeza nao nafasi ikitokea,sio wanaokupa maneno mengi pasipo kushauri kujijenga.
8.Watafute marafiki wanaopenda kuona ukikua vizuri katika maeneo mengine,sio watakaokuona kama mwiba katika ukuaji wao
9. Watafute wanawake marafiki wanao heshimu maisha yako ya ndoa na mahusiano,sio wanaokushauri kuwachana na mume wako.
10. Watafute waanawake marafiki watakao kunoa kufikiri kwako sio wanaozungumzia urembo wako pekee.
11.Watafute wanawake marafiki watakao kubariki sio watakaokutumia vibaya
12. Watafute marafiki ambao watakutuliza wakati umefikia kufanya maamuzi mabaya maishani,au watakaokuona ukifanya maamuzi mabaya ukiwa katika changamoto.
13. Watafute marafiki amabao wataweka siri yako iwe siri sio watakuanika.
Cantona School of Thoughts
Tembea Youtube Subscribe Youtube channel yangu
CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4
Website: cantonadigital.wordpress.com
Email:cantona.online254@cantonajoseph
#MahusianoNaNdoa #IpoSiku #marriagemathematics #FamiliaNaMalezi #MaendeleoNaMafanikio#CantonaJoseph
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.