
Wakati unapogombana na mpenzi wako kila siku hapo nyumbani fahamu watoto wako wanasikia.
Wakati unapoamua utalala katika chumba tofauti,fahamu watoto wenu wanaliona.Wakati unapoamua kwamba hautaomba,huku unajifanya mnaomba pamoja wakati wageni wapo nyumbani watoto wanalifahamu.
Wakati unapoamua hautatenga mda spesheli wa kuwa pamoja na mpenzi wako,watoto wako wanaliona hilo.Wakati woowote unapoongea vibaya kwa mpenzi wako,watoto wako wanasikia hayo.Kila wakati unapomkasirisha mke/mme wako,anapotokwa na machozi watoto wako wanayaona.
Wakati hamna amani,hapo nyumbani baina yenyu wawili watoto wanaliona.Wakati wote mnapogombana kwa ahata mambo madogo madogo watoto wanayaona.Wakati mnapovutana kuhusu malezi ya watoto watoto wanayaaona.
Wakati unapokuja nyumbani ukiwa umechelewa,unakwepa kichuna chako watoto wanayaona.
Unapoamua utaishi katika ndoa kwa sababu ya watoto tuu,huku upendo baina yenu ukiwa umepoa fahamu watoto wanalionaUnapoamua kuficha maswala baina yenu,huku mkiona ni sawa,watoto wanayaaona na wanaogopa kuyasema,vitendo kama hivi vinaleta changamoto katika ukuaji wa watotoMatendo kama haya si msingi bora kwa kizazi chako,iwapo unawajali watoto wako basi ni bora,kuepuka matendo kama haya.
Ni bora watoto wako kuwa na makuzi katika mazingira yenye upendo,furaha,amani,ulinzi,umoja,ushirikiano,na kumbukumbu yenye matumaini.Hii ndio zawadi nzuri unaweza ukampa mpenzi wako na watoto,maana mlianza familia wawili,Mungu akawajalia watoto ambao hawahitaji kupitia machungu unayoyaleta katika ndoa kila kukicha.
Cantona School of ThoughtsTembea Youtube
Subscribe Youtube channel yangu CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4
Website: cantonadigital.wordpress.com
Email:cantona.online254@gmail.com#MahusianoNaNdoa#IpoSiku#marriagemathematics#FamiliaNaMalezi#MaendeleoNaMafanikio
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.