
1.Wote wawili wanahitaji heshima.Heshima sio ya mwanaume pekee yake.
2. Wanandoa wote wanahitaji kumegana.Swala ya kujamiana si la mtu mmoja,ni swala ya wawili mke na mme,likifanyika ndani mwa ndoa lina ubora wake.
3.Wapenzi wanahitaji usalama,wakati mwanaume anajitahidi kutoa ulinzi,alipoamua kuoa ni ishara tosha mwanaume alipata mwanamke wa ndoto zake,hili linadhibitisha pendo lake kwako.Anahitaji nawe kumwakikishia upo naye katika safari yake maisha.
4.Wote wawili wanahitaji kupongezwa,wewe dada unatamani mwanaume akupee pongezi kwa juhudi zako,iwapo umetekeleza swala kubwa au ndogo.Naye ujihisi vizuri unapofanya hivyo kumpongeza.
5. Wote wawili wanahitaji upendo.Wanaume wengi,hawalifaulu hilo wanaume wengi huanza kununua zawadi.Fahamu mwanamke atakupenda.Wanaume wengi huwa wanaogopa kuachwa na mwanamke anayempenda,Ukweli mwanamke anaweza kuonyesha heshima kutokana na hadhi uliyo nayo katika jamii,huku anamdharau moyoni.Ila mwanamke atamweshimu mwanaume wa ndoto zake.Mwanamke aliye megana nawe atakuonyesha heshima.
6. Wote wanahitaji kueleweka,hamna kitu ambacho kinaudhi sana kama kutoelewana,wote wawili wanahitaji kuelewa hilo.Hakuna kitu kinaumiza moyo iwapo mpenzi wako atatoa kuhukumu kutoka na kuhisi tuu umechelewa,unakisia tuu,si jambo njema kukisia jambo ambalo mwenzako hajalifanya.
7. Wanaopendana wanahitaji uwaminifu,jinsi ilivyo haupendi uzinifu ishi maneno yako uwaminifu muhimu,maana hautapendelea iwapo mke/mwanaume wako ni msherati kamwe hautakubali.
8. Wote wanalihitaji neno nakupenda,mwanamke anapogundua siku za hivi karubuni huvitumii hivyo basi inakua ni balaa,pendo unaweza ukalisema,anasubiria kusoma ujumbe wako,anasubiri kupokea simu yako.
9.Swala la kumjulia hali mwenzako linahitajika kuwa vizuri kwenye hili eneo.Wacha akakuone ukiwa mtu unaweza hilo unamfikiria.
10. Wote hawapendi kudhulumiwa na kukosewa. Hamna anayetaka mwanamke wake kuhangaika.Usiwai mpiga mwenzako,kumdharau na kusema vibaya.
11. Omba msamaha iwapo ni wewe umefanya makosa,usifunikie makosa.
12.Lea malengo/maono ya mwenzako,maana mnapendana,taka kujua ndoto zake maishani.
13.Wote wanahitaji mwenza,hadi milele ni safari ndefu,mazungumzo yanahitajika,usifanye mwenzako ashindwe kuzungumza.
14.Uwaminifu ni jambo muhimu kwa wote wawili,pasipo uwaminifu iwapo hamna uwaminifu.Upendo sio kuwaza wewe pekee ni kumjali na mwenzako.Mtendee mwenzako unachotaka nawe akutendee,usiwe na ubinafsi.
Cantona School of ThoughtsTembea
Youtube Subscribe Youtube channel yangu CantonaCast Television https://youtu.be/kFruH4ysPE4
Website: cantonadigital.wordpress.com
Email:cantona.online254@gmail.com
#MahusianoNaNdoa#IpoSiku#marriagemathematics#FamiliaNaMalezi#MaendeleoNaMafanikio#CantonaJoseph
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.