Ukatili wa kingono sehemu ya “maisha ya kila siku” katika baadhi ya maeneo Sudan: MSF

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 31, 2026 18:00 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader
xcv

Vitendo vya ubakaji na ukatili wa kingono bado ni “sehemu ya maisha ya kila siku” katika maeneo ya Sudan hata pale ambapo mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yamepungua, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kimataifa la madaktari wasio na mpaka Médecins Sans Frontières (MSF).

Ripoti hiyo inaeleza kuwa ubakaji umekuwa “sifa kuu” ya mzozo huo, ambapo mashambulizi mengi hutekelezwa na wanaume wenye silaha na mara nyingi huambatana na ukatili mkubwa pamoja na udhalilishaji.

Hata hivyo, MSF inasema kuwa ubakaji umeendelea kama sehemu ya maisha kwa siri katika jamii za eneo la magharibi la Darfur, hata katika maeneo ambayo hayapo tena katika mstari wa mbele wa mapigano.

Ripoti hiyo ndiyo uchambuzi wa kina zaidi hadi sasa kuhusu ukatili wa kingono katika vita vya Sudan ambavyo vimekaribia kuingia mwaka wa tatu.

Onyo:Habari hii ina maelezo ya ukatili wa kingono ambayo yanaweza kuwa ya kusikitisha kwa baadhi ya watu.

Ripoti hiyo inabainisha ushuhuda wa waathirika 3,396 waliotafuta matibabu katika vituo vinavyoshirikiana na MSF katika eneo la Darfur Kaskazini na Kusini kati ya Januari 2024 na Novemba 2025.

Pande zinazopigana jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) zote zinatuhumiwa kufanya ukatili wa kingono.

Hata hivyo, Darfur ni ngome ya RSF, na idadi kubwa ya wahalifu waliotambuliwa na manusura walikuwa wapiganaji wa kundi hilo.

Visa vingi vilivyotajwa katika ripoti hiyo vilitekelezwa katika eneo lenye migogoro mikali la Darfur Kaskazini mwaka uliopita, kufuatia RSF kuchukua udhibiti wa kambi za wakimbizi za Zamzam na Abu Shouk, pamoja na mji wa el-Fasher mwezi Oktoba ambapo MSF inaeleza hali hiyo kuwa “moja ya matukio ya kutisha zaidi, yenye ukatili usioelezeka”.

Serikali ya Taliban yataka kuongeza uagizaji wa mafuta kutoka Urusi

xcv

Maafisa kutoka wa Urusi wamesema kuwa serikali ya Taliban nchini Afghanistan imeomba kuongeza kiwango cha mafuta inachoagiza kutoka Urusi hadi tani milioni mbili kwa mwaka.

Shirika la habari la serikali ya Afghanistan, Bakhtar News Agency, limemnukuu mkuu wa kituo cha biashara cha Urusi, Rustam Khabibulin, akisema: “Afghanistan imependekeza kununua tani milioni mbili za bidhaa za petroli kutoka Urusi kila mwaka kwa muda mrefu.”

Afisa huyo wa Urusi alisema kuwa nusu ya makubaliano hayo ya biashara itakuwa gesi asilia iliyoyeyushwa (LNG), huku sehemu iliyobaki ikiwa ni petroli na dizeli.

Mkuu huyo pia alieleza matumaini yake kuwa makubaliano hayo yatasainiwa na baadhi ya kampuni kubwa za Urusi.

Kwa mujibu wa ripoti, mauzo ya mafuta kutoka Urusi kwenda Afghanistan yameongezeka kwa asilimia 20 katika mwaka uliopita.

Aidha, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni ya Energostar Trading, nchi ya Belarus imesafirisha tani 400,000 za mafuta kwenda Afghanistan mwaka huu pekee.

‘Nendeni mukachukue mafuta yenu wenyewe kutoka Mlango-Bahari wa Hormuz – Trump

.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi “kama Uingereza” ambazo haziwezi kupata mafuta ya ndege kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa kuhusiana na Mlango Bahari wa Hormuz zinapaswa “kuwa na ujasiri ambao umeshachelewa, kwenda kwenye Mlango Bahari, na KUCHUKUA tu”.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Truth Social, aliandika kwamba nchi “zitalazimika kuanza kujifunza jinsi ya kujipigania, Marekani haitakuwapo kuwasaidia tena, kama vile ambavyo hamkuwepo tulipowahitaji,” akizungumzia nchi “ambazo zilikataa kushiriki katika vita vya Iran”.

“Kimsingi, Iran imeangamizwa kabisa. Sehemu ngumu imekamilika,” ujumbe huo uliongeza, ukiishia na: “Nendeni mukachukue mafuta yanu mwenyewe!”

Ufaransa ‘haisaidii sana’, Trump asema katika ujumbe uliofuata

Katika ujumbe uliofuata alioutuma kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema Ufaransa “haikuruhusu ndege zinazoelekea Israel, zenye vifaa vya kijeshi, kupaa juu ya eneo la Ufaransa”.

Aliendelea kusema Ufaransa “imekuwa haina msaada wowote kwa ‘Iran anayechinja watu,’ ambayo imesambaratishwa!”

Ujumbe huo unahitimishwa na rais wa Marekani akisema: “Marekani ITAKUMBUKA!!!”

Fahamu mambo manne kuhusu vita vya Marekani, Israel dhidi ya Iran

XCV
Maelezo ya picha,Mwanamume akibeba masanduku kutoka nyumba iliyoharibiwa kwa shambulio mjini Tehran siku ya Jumatatu

Vita vitaisha lini?

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa vita kati ya Marekani, Israel dhidi ya Iran “vimevuka zaidi ya nusu ya safari,” ingawa baadaye alifafanua kuwa alimaanisha kwa upande wa operesheni za kijeshi, si muda halisi wa vita.

Netanyahu aliongeza kuwa vita hivyo vimesababisha vifo vya “maelfu” ya wanajeshi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC), na kwamba Israel pamoja na Marekani wako “karibu kumaliza kabisa sekta ya silaha” ya Iran, ikiwa ni pamoja na kuharibu viwanda muhimu na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

Mashambulizi yanaendelea katika ukanda wote

Wakati huo huo, mashambulizi yanaendelea katika maeneo mbalimbali.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema limeanzisha wimbi jipya la mashambulizi katika mji mkuu wa Iran, Tehran, saa chache baada ya kubaini makombora yaliyotumwa kutoka Iran kuelekea Israel.

Mashambulizi pia yameripotiwa katika eneo la Ghuba, ikiwemo Dubai, ambako mamlaka zimesema meli ya mafuta iliteketea kwa moto kufuatia shambulio la ndege isiyokuwa na rubani kutoka Iran.

Mpango wa Iran wa kutoza ushuru katika Mlango-Bahari wa Hormuz

Kwa upande mwingine, Iran inapanga kuweka ushuru kwa meli zinazopita katika mlango wa Bahari wa Hormuz.

Ripoti zinaeleza kuwa meli za Marekani na Israel, pamoja na zile za nchi zilizoshiriki kuiwekea Iran vikwazo, zitazuiwa kupita katika mlango huo muhimu wa bahari.

Rubio asema njia hiyo ‘itafunguliwa tena kwa namna moja au nyingine’

Naye Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani, Marco Rubio, amesema kuwa mlango huo wa Hormuz “utaendelea kufunguliwa kwa njia moja au nyingine,” akisisitiza umuhimu wake kwa biashara ya kimataifa.

Idadi ya vifo yaendelea kuongezeka kufuatia vita kati ya Marekani, Israel dhidi ya Iran

XCV
Maelezo ya picha,Mazishi katika makaburi ya Behesht Zahra kusini mwa Tehran tarehe 26 Machi.

Tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani, Israel dhidi ya Iran tarehe 28 Februari, idadi ya vifo imeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati.

Iran:Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Iran la Human Rights Activists in Iran (HRANA) linaripoti kuwa watu 3,492 wameuawa tangu vita vianze. Kati yao, raia ni 1,574, wakiwemo takriban watoto 236.

Israel: Shirika la huduma ya dharura la Magen David Adom (MDA) linasema watu 19 wamefariki kutokana na mashambulizi ya makombora tangu vita kuanza. Aidha, wanajeshi tisa wa Israel wanaripotiwa kuuawa nchini Lebanon, kwa mujibu wa jeshi la Israel.

Lebanon: Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu 1,247 wameuawa, wakiwemo watoto 124.

Nchi za Ghuba: Kwa ujumla, watu wasiopungua 24 wamefariki katika nchi za Ghuba. Wengi wao ni maafisa wa usalama au wafanyakazi wa kigeni.

  • Umoja wa Falme za Kiarabu: vifo 11
  • Kuwait: vifo 7
  • Oman, Saudi Arabia na Bahrain: kila moja imeripoti vifo 2

Hali inaendelea kuwa tete huku idadi ya waliopoteza maisha ikiongezeka kila siku kutokana na mapigano yanayoendelea

katika eneo hilo.

Kamanda mstaafu wa jeshi asema matumizi ya nguvu hayataleta suluhisho Hormuz

xcv

Kamanda mstaafu wa jeshi la wanamaji, Tom Sharpe, amesema anaamini kuwa Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni mojawapo ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta, hauwezi kufunguliwa kwa kutumia nguvu kama ambavyo Marekani imetishia kufanya.

Akizungumza na kipindi cha Today cha BBC Radio 4, Sharpe amesema kuwa Kama Iran haitakubali kuacha kushambulia boti zinazopita hapo, basi kutumia nguvu kupambana nao hakutafanikiwa.

“Iran ina udhibiti wa hali hii, hilo liko wazi, na naamini wataendelea kuwa nao hata katika siku zijazo,” amesema Sharpe, akiongeza kuwa si kwa manufaa yao kubadili msimamo huo kwa sasa.

Amesema pia kuwa hatma ya hali hiyo inategemea uamuzi wa Iran katika wiki au miezi ijayo.

Meneja wa timu ya Ghana Addo, apigwa kalamu

.
Maelezo ya picha,Ghana ilishindwa kufuzu Afcon 2025 chini ya uongozi wa Addo

Ghana imefuta kazi meneja wa timu ya taifa hilo Otto Addo, siku 72 tu kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia.

Kuondoka kwa Addo kunajiri baada ya timu ya Black Stars ya Ghana kushindwa 2-1 na Ujerumani katika mechi ya kirafiki mjini Stuttgart siku ya Jumatatu, na pia kupokea kichapo cha 5-1 na timu ya Austria mjini Vienna Ijumaa iliyopita.

Timu ya Black Stars ambao wapo katika kundi moja na timu ya Uingereza, wamepoteza mechi nne walizocheza hivi karibuni, licha ya kuwa na winga wa Manchester City Antoine Semenyo na mshambuliaji wa Tottenham Mohammed Kudus, licha ya kuwa nao walishindwa kuhitimu katika mashindano ya kombe la Africa Afcon chini ya kocha Addo.

Baada ya mechi ya Ujerumani, shirikisho la soka la Ghana lilisema kuwa “wameachana na Addo” na “ataondoka mara moja”

Shirikisho hilo liliongeza kuwa “tutatoa taarifa kuhusu mwelekeo mpya utakaochukuliwa na timu ya Black Stars”

Addo, mwenye umri wa miaka 50, alizaliwa nchini Ujerumani na alichezea taifa hilo. Akiwa kocha wa Ghana wameshinda vikombe 15 chini ya uongozi wake, na alikuwa ameanza muhula wake wa pili kama meneja kuanzia Machi 2024.

Michuano ya kombe la dunia yatafanyika nchini Canada,Mexico na Marekani kuanzia tarehe 11 mwezi Juni hadi tarehe 19 mwezi Julai.

Ghana itaanza na kuchuana na Panama tarehe 18 mwezi Juni kabla ya kukabiliana na Uingereza tarehe 23 mwezi Juni na kisha Croatia tarehe 27 mwezi huo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply