Mwenye nguvu huwalinda wasio na nguvu, tajiri kwa ajili ya maskini, mwenye nacho kwa ajili ya wasio nacho, na mwenye hekima kwa ajili ya wasio na hekima, hii ndiyo kanuni ya maisha isiyokwepeka ambayo Mungu ameiweka makusudi ili tuweze kushirikiana.
Matajiri wote unaowaona leo duniani tafsiri ya utajiri wao inatokana na baraka zao kuwanufaisha masikini na hii ni iwe wanataka au hawataki, iwe kwa kujua au kutokujua.
Kwa mfano tukianza na nyumba nzuri uliyoijenga anaeifaidi zaidi ni house girl au house boy uliyemuajiri kutoka shamba ambaye anatumia muda wake mwingi ndani ya siku nzima akiwa ndani ya nyumba hiyo wakati wewe hauna muda mwingi wa kukaa na kuifurahia maana unatoka asubuhi na kurudi usiku
Ni kweli una pesa nyingi kwenye bank account yako lakini pesa hizo zipo kwa ajili ya kuwapa watu wanaokutumikia katika miradi yako ambapo ili ziongezeke ni lazima zipite mikononi mwao maana hauwezi kuzitumia mwenyewe bila watu wengine kuzigusa maana kanuni ya maisha haikuruhusu, kweli ni zako lakini kuna waalimu wanaofundisha watoto wako wanazingojea ili ziwalipe mshahara, bado hujatoa chakula cha wafanyakazi wa shamba, chakula cha mifugo nk, na ili uendelee kuongezeka ni lazima uruhusu zipite katika njia hiyo ya kuwekeza kwenye miradi ambayo itatengeneza ajira kwa wasiokuwa na ajira ndipo faida iweze kukurudia
Kukua na kuongezeka kwako kunategemea sana idadi ya watu wanaoishi kupitia juhudi za mkono wako na endapo hauna watu wanaokutegemea basi utakuwa miongoni mwa masikini wasiojiweza maana ahadi ya Mungu ni pamoja na kukuzidishia watu watakaokutumikia na kukutegemea yaani watu wanaoishi kupitia wewe.
Hili swala siyo katika umiliki wa mali pekee bali kila ongezeko katika maisha linaendana na kutegemeana kwa mfano kuna vitu alivyonyimwa mwanamke na akapewa mwanaume kadhalika alivyonyimwa mwanaume akapewa mwanamke ambavyo hivi ndiyo husababisha kila mmoja amuhitaji mwenzake na hapo hata uwe na pesa au madaraka kiasi gani ili upate ambacho hauna ni lazima uwe mpole na mnyenyekevu na utumie lugha ya uungwana na staha
Ni kweli umesoma lakini kuna wakati utawahitaji mbumbumbu ambao hawajasoma, nikupe mfano mdogo tu, gari yako nzuri ya gharama ikikuzimikia ghafla barabarani sidhani kama muda huo utamuhitaji profesa au daktari wa sheria bali utawahitaji hawahawa akina bwakila ili wakusaidie kusukuma gari.
That is how the way it is na yeyote mwenye kufanikiwa ni yule mwenye kukubali kuenenda sawasawa na kanuni hii ambayo Mungu ametuwekea.
Napenda utumie muda huu kujitafakari, ni watu wangapi wanaishi mjini kupitia nguvu zako?! I mean umeajiri watu wangapi ambao kila mwisho wa mwezi pesa yako inawafanya wao na familia zao watabasamu, maana hicho ndiyo kipimo kikuu cha mtu aliyefanikiwa
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.