Pambania ndoto yako….

Mchakato kwenye kuelekea ndoto yako, unaweza kuwa sio wakufurahisha sana!Usigeuke nyuma! Kaza mwendo !Mchakato unaweza kuonekana kama hakuna mwelekeo kwa unachokiiota!

Wewe kaza tu kupambania ndoto yako.Nimejaribu kujizuia! Ila nimeshindwa… kuna wewe unahisi ulichokitarajia hukioni!Ila una ndoto na sauti ya ndani inasema utatoboa…. ila Mazingira hayakuoneshi kama kuna ushindi;Mchakatoni, huwa sio pashangwe sana wakati mwingine!Anapotaka kuzaliwa mtoto ule uchungu ule.. wamama wanaelewa zaidi..Kubeba ujauzito pia! Kuna milalo mtu halali kwa miezi Tisa..

Mtoto akizaliwa ni furaha mno!Vumilia mchakato mtoto ndoto yako atazaliwa tuu! Utasahau;Mchakato utabakia historia tu!SONGA MBELEE; Best, Futa machozi!

Mtoto ndoto yako atazaliwa tu;Acha mchakato ukuchakaze! Fine Sawa eee,, ukiwaza mtoto ndoto atakavyokuwa mzuri..Pata nguvu uendelee kusubiria Hata kama ujauzito wamtoto ndoto ndo kwanza unawiki tatu, tambua miezi tisa itafika IPO SIKU;


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment