Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa: March 25, 2026 04:27 (EAT)



Rais wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Mike Schmidt/photowerkstatt/picture alliance
Steinmeier ashambulia Marekani kwa vita dhidi ya Iran, na kusema hakuna haja kwa Ujerumani kuegemea upande wa Trump
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amekosoa vikali vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iranakivitaja kuwa ni ukiukwaji wa sheria ya kimataifa.
Kwa maneno mazito na yasiyo ya kawaida kwa Marekani ambayo ni mshirika wa muda mrefu wa Ujerumani, Steinmeier amesema kuna mgogoro mkubwa mno na imani katika siasa za Marekani imepotea, sio tu miongoni mwa washirika wetu bali duniani kote.
Steinmeier aliongeza kuwa hakuna sababu yoyote kwa nchi yake kuegemea upande wa Rais Donald Trump. Amesema hayo mjini Berlin kwenye maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa upya kwa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
“Vita hivi, na tafadhali nisamehe kwa kusema hivyo kama mtu aliyehusika moja kwa moja, ni kosa la kisiasa lenye madhara makubwa. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba hivi ni vita vinavyoweza kuepukwa kabisa na visivyo vya lazima, ikiwa lengo lake lilikuwa kweli kuzuia Iran isiendelee kutengeneza silaha ya nyuklia,” amesema Steinmeier.
Ingawa wadhifa wa Steinmeier hauna uzito mkubwa kisiasa, kwa kiasi kikubwa, maneno yake yana uzito nchini Ujerumani, ambayo haijalaani rasmi vita dhidi ya Iran.
Ghana, EU zasaini mkataba rasmi wa ulinzi

Makamu wa rais wa Ghana, Ghana Jane Naana Opoku-AgyemangPicha: Fatemeh Bahrami/AA/picture alliance
Ghana na Umoja wa Ulaya zimesaini mkataba rasmi wa kwanza wa ushirikiano wa ulinzi.
Mkataba huo umesainiwa mjini Accra na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas na makamu wa rais wa Ghana Jane Naana Opoku-Agyemang.
Unalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za kukabili ugaidi, kuimarisha intelijensia na kukabili mizozo.
Makubaliano hayo yamesainiwa wakati mataifa ya Afrika Magharibi yanatafuta njia za kuzuia kuenea kwa ghasia kutoka kanda ya Sahel, ambapo makundi yenye silaha yenye mafungamano na Al-Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiislamu (IS), yameongeza mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni.
Urusi yavurumisha takriban droni 400 dhidi ya Ukraine

Watu wanne wameuawa na 27 kujeruhi nchini Ukraine baada ya Urusi kuvurumisha mamia ya droniPicha: REUTERS
Urusi imevurumisha mamia ya droni na makombora kulenga mji mkuu wa Ukraine Kiev na miji mingine, na kusababisha maafa.
Mashambulizi makubwa ya droni na makombora kutoka Urusi dhidi ya maeneo ya raia nchini Ukraine, yamewaua watu wanne na kujeruhi wengine 27.
Maafisa nchini Ukraine wamesema hayo siku ya Jumanne mnamo wakati jeshi la Moscow likiongeza juhudi za kuvunja mstari wa mbele wa Ukraine vitani, katika kile kinachoweza kuwa mwanzo wa shambulio la ardhini lililotarajiwa la majira ya machipuko.
Jeshi la angani la Urusi limesema Urusi ilivurumisha takriban droni 400 za masafa marefu dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia Jumanne.
Mashambulizi hayo ambayo ndiyo makubwa zaidi katika wiki ya hivi karibuni, yalirindima hadi mapema siku ya Jumanne ambapo mji mkuu Kiev pia ulilengwa.
Mafuriko yaongezeka Kenya, idadi ya vifo yafika 88

Serikali ya Kenya yatoa tahadhari kwa raia wake kuhusu mafurikoPicha: Boniface Muthoni/SOPA Images/Sipa USA/picture alliance
Serikali ya Kenya imesema mito miwili imevunja kingo zao kwa sababu ya mafuriko na kulazimisha familia kadhaa kuhama makwao.
Kufuatia hali hiyo, idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini humo imeongezeka na kufika 88.
Takriban kaunti 21 zimeathiriwa na mafuriko, hali inayozusha wasiwasi kuhusu usalama wa umma, uharibifu wa miundombinu na ongezeko la misaada ya kibinadamu.
Kulingana na wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, idadi ya watu ambao wameyakimbia makaazi yao tangu mafuriko hayo yaanze mapema mwezi Machi, imefika 34,000.
Kisa cha hivi karibuni zaidi kimetokea Magharibi mwa Kenya ambapo mto Nyando ulifurika jana Jumatatu na kufunika sehemu ya daraja ya Ahero katika Barabara kuu ya Kericho-Awasi-Kisumu, hali iliyovuruga usafiri katika eneo hilo.
Zaidi ya raia 500 waliuawa kwenye mashambulizi Sudan

Umoja wa Mataifa waelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la mashambulizi ya droni katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya SudanPicha: Wang Hao/Xinhua/IMAGO
Zaidi ya raia 500 waliuawa kwenye mashambulizi ya droni nchini Sudan kati ya Januari na Machi 2026.
Umoja wa Mataifa umesema hayo leo Jumanne na kuongeza kuwa mauaji mengi yalitokea katika jimbo la kimkakati la Kordofan.
Shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limesema kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya droni katika vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan.
Msemaji wa shirika hilo Marta Hurtado amewaambia waandishi Habari mjini Geneva kwamba katika wiki mbili za kwanza za Machi pekee, taarifa zilizopokelewa zinaonyesha kuwa zaidi ya raia 277 waliuawa. Zaidi ya robo tatu yao waliuawa katika mashambulizi ya droni.
Aliangazia hasa shambulio la tarehe 20 Machi dhidi ya Hospitali ya El-Daein, katika jimbo la Darfur Mashariki, lililoua watu 70, wakiwemo watoto 13, na kujeruhi wengine 146.
Iran yaendeleza mashambulizi dhidi ya Israel na majirani

Wazima Moto wakizima moto baada ya shambulizi la Iran lililoharibu jengo mnamo Machi 24, 2026 mjini Tel Aviv nchini Israel.Picha: Erik Marmor/Getty Images
Iran imeendelea na mashambulizi yake dhidi ya Israel na nchi za Kiarabu za Ghuba siku ya Jumanne.
Iran imeendelea na mashambulizi yake dhidi ya Israel na nchi za Kiarabu za Ghuba siku ya Jumanne, huku kombora moja likishambulia barabara katikati ya mji wa Tel Aviv nchini Israel.
Mwandishi wa shirika la Habari la AP aliyekuwa katika eneo la shambulio la makombora ya Iran dhidi ya Tel Aviv aliona shimo kubwa ardhini mapema leo kutokana na shambulio hilo.
Afisa wa idara ya zima moto na uokoaji wa Israel katika eneo la shambulio Avi Gabbay amesema “kwa bahati nzuri, hakukuwa na vifo wala majeruhi vilivyopatikana katika majengo. Kwa ujumla, ilikuwa ushirikiano bora kabisa pamoja na vikosi vyote washirika, ikiwa ni pamoja na polisi.”
Haya yanajiri licha ya rais wa MarekaniDonald Trump kusema jana kwamba Marekani iko katika mazungumzo na Jamhuri hiyo ya Kiislamu kumaliza vita ambavyo vimetanuka kote Mashariki ya Kati.
Trump pia alisitisha kwa siku tano tarehe ya mwisho kwa Irankufungua njia ya mlango wa Bahari Hormuz kwa usafirishaji wa meli la sivyo vituo vyake vya umeme vishambuliwe.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.