Kuna kuinuka tena usikate tamaaKuna kipindi katika maisha unaweza kukipitia na kikasababisha moyo wako kuinama kwa kiwango cha maisha yako kukosa radha na maana ya kuishi Katika kipindi cha namna hii unaweza kukutana na mambo mengi ya kukuvunja moyo kwa kiwango cha moyo kuvuja damu japo waliokuzunguka wanaweza wasielewe kwa ukubwa kiwango cha maumivu unayo yapata Maono na ndoto zote huzimika kama mshumaa katika kipindi hiki,furaha nakicheko hukoma gafla, huzuni na kilio hutanda kwenye moyo wako na simanzi iliyojaa sauti ya why me !!!!!! Kwanini mimi tu? Niliwahi kuomba na dada mmoja aliyewahi kuchumbiwa na wanaume kama watano na kila mmoja alikuwa anamuahidi kumuowa lakini kila mmoja alikuwa anamkimbia bila maelezo mazuriHaya mazingira yalimuumiza sana kiwango cha kukata tamaa na kuona labda yeye alizaliwa na mikosi hana bahati kama wengine, alikuwa na ndoto nyingi lakini kutoka na aliyoyapitia zilizima kama mshumaa Alifika mahali pa kujichukia na alitamani muda wote kujitenga na wanadamu maana alijiona yeye hana bahati na wala sio kama wanadamu wengine Yawezekana na wewe ni kama huyu dada umepitia vitu vingi sana vya kuumiza na vya kujeruhi moyo wako. Hakuna siku kwenye maisha yako umewahi kupata furaha na afadhari ya Jana kuliko ya leo Mungu amenituma kukwambia jifunze kujipa muda kuna wakati wa kulia lakini pia kuna wakati wa kucheka si nyakati zote utakuwa mtu wa kulia kuna wakati wa kucheka pia Nataka nikwambie baada ya maombi Mungu alimwinulia mtu aliyempenda na kumfuta machozi wakafunga ndoa yao nzuri na Mungu akawainua kwa kiwango ambacho wale waliomzadharua huyu dada na wakamkimbia bila maelezo walimsalimia kwa heshima Ninakuombea Mungu afanye na kwako pia Yule Mungu aliyefanya kwa wengine na kwa huyu dada afanye na kwako pia na ninaona Mungu akikufuta machozi na kukupa furaha na kicheko katika jina la YesuAmini tu usikate tamaa kuna kuinuka tena hautalia nyakati zote kuna wakati wa kuinuka tena na kucheka, kuna kuinuka tena
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.