Katika maisha tumezungukwa na watu wauwa ndoto na hawa watu kazi yao ni kukukatisha tamaa katika yale mawazo sahihi uliyonayo ya kuifikia hatima yako au malengo yako .Na mimi leo nataka utafakari umezungukwa ns watu wa aina gani wanaokutia moyo na kukwambia unaweza au wanaokutisha na kukukatisha tamaa kila wakati .Jambo hili limewakwamisha wengi kutokuyaishi malengo maono yao. Una maono makubwa unauwezo mkubwa lakini umezungukwa na watu wanaokukatisha tamaa na kukwambia huwezi .Usipojifunza kuamini katika uwezo wako binafsi na kuamua kufunga masikio na kuendelea mbele itakuwa ngumu Sana kwako kuifikia ndoto yako 1samweli 17:32:33 Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake. Hapa nataka tuangalie mambo mawili1. Sauli na Jeshi lake walitamani sana kumpiga Goliath ili kuonesha uwezo wa hilo jeshi lakini kutokana na ukubwa wa Goliath walivunjika moyo na wakaogopa Sana na wakajiona hawana uwezo hata kidogo wa kumpiga Goliath watu Kama hawa tunaowengi kwenye jamii mambo wanavitu wanatamani kufanya lakini kutokana na ukubwa wa hivyo vitu wamekata tamaa na kuvunjika moyo na kuona hawawezi tena 2. Sauli na Jeshi lake ndio waliogeuka kuwa washauli wa Daudi
cheki washauli wako wamempiga Goliath au wameshindwa? na ikiwa wameshindwa unafikili watakushauli nini zaidi watakukatisha tamaaa tu. Ndio maana sauli na Jeshi lake walimkatisha tamaa Daudi kwamba wewe ni kijana mdogo huyu mtu tumemshindwa sisi wewe utaweza anapigana vita tangu ujana wake sisi wakubwa zako tumekimbia .Nataka nikwambie Kama wamekimbia kivyao vyao wewe unaweza songa mbele hakuna kukata tamaa, Ukubwa wa Goliath uzoefu wa Goliath wako usikutishe jiwe moja laweza kumpiga na kumuuwa .Azimie moyo mtu kwa ajili ya upinzani unaokutana nayo Mungu amenituma nikutie moyo unaweza usiogope songa mbele hata Kama umekatishwa tamaa ukaona huwezi Bwana amenituma nikwambie usiogope unaweza
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.