Usimfiche mke wako

Unamficha mke wako amekuwa bangi? Au amekuwa madawa ya kulevya?!! Biblia inasema, “Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua”. (Mhubiri 9:9).
Kama unamfurahia mkeo hauwezi kumficha, maana moja ya furaha ni pamoja na kumpost ili watu wamuone, Ila kama uko nae kwa maslahi binafsi hapo lazima afichwe tu.
Mfalme Ahasuero alimpenda na kumfurahia sana mke wake, katika kitabu cha Esta 1:10-11 imeandikwa, “Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero,
wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso”.
Mfalme baada ya kupiga gambe na kufurahi aliingia kwenye uhalisia na kutaka kuwaonyesha watu kwamba mbali na cheo chake, pamoja na utajiri anaomiliki, furaha yake nyingine kubwa ni mke wake ambaye ni mzuri na mrembo.
Huu ndiyo moyo mwanaume, akiwa anakupenda na anakufurahia hawezi kukuficha but ukiwa na kasoro ambazo hazikidhi vigezo vyake hapo lazima ufichwe na mimi nasema kwamba utafiti
Kumpost mkeo ni namna ya ku present furaha yako na wala sio ushamba au ulimbukeni, wachana na maneno ya magumegume yasiyokuwa na mahusiano ya furaha, wewe kama una furaha be free and be happy with your love….


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment